Pichani ni mnara wa kumbukumbu ya eneo ambalo walizikwa watu waliopoteza maisha katika ajali ya MV Bukoba hiyo mnamo Mei 21.1996.
Kila mwaka ifikapo Mei 21, kama siku ya leo watanzania tunakumbuka tukio la ajali mbaya iliyowahi kutokea katika nchi yetu ya kuzama kwa meli ya MV Bukoba ndani ya ziwa Victoria, mnamo mwaka 1996. Kwa hali hiyo watanzaia tunaendelea kuwaombea ndugu na jamaa waliotangulia mbele za haki.
Mtandao wako bora wa habari wa #RoryaFinestBlog, unaungana na watanzania wote popote walipo kwa pamoja kuwaombea mema waliotangulia mbele za haki katika ajali hiyo, mbaya kabisa nchini mwetu.
Pia mishumaa ya amani na upendo kwa ndugu na familia tunaiwasha kwa pamoja siku hii ya leo na mwisho tunamalizia kwa kusema ‘AMEN’.
Ajali ya kuzama kwa Mv Bukoba ilitokea katika ziwa Victoria mnamo tarehe 21/5/1996 na kupoteza maisha ya zaidi yawatu 1000. Ambao baadhi yao walizikwa katika kaburi la pamoja.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena