Julius Mtatiro wa CUF ambaye analiwania jimbo la Segerea …kupitia UKAWA
Na Andrew Chale, modewjiblog
(Dar
es Salaam). Mnamo Agosti 2.2015, Aliyekua Kada wa Chama cha Mapinduzi
(CCM), Dk. Milton Makongoro Mahanga ametangaza rasmi kujiunga na
upinzani kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).. hata
hivyo baada ya kutangaza huko tayari wanasiasa mbalimbali wamekuwa na
maoni yao huku wengine wakimtaka akubali ushindani ndani ya UKAWA.
Miongoni
mwa wanasiasa hao ni pamoja na Kada wa CUF Mwanasheria na mchambuzi wa
mambo ya siasa nchini, Julius Mtatiro ambaye ameonyesha nia ya kulitaka
jimbo hilo kipindi kirefu kupitia CUF na umoja wa UKAWA, ametoa ujumbe
mzito wa kumkaribisha kada huyo ‘mjeruhiwa wa CCM’.
Julius Mtatiro kupitia ukurasa wake wa facebook, aliandika:
“Comrade Makongoro Mahanga! Karibu sana UKAWA!!…Kama unalitaka jimbo la Segerea njoo tushindanishwe kwa sifa uwezo na vigezo.
Natambua
utakuwa na mchango mkubwa sana kwa ushindi wa UKAWA lakini lazima uwe
tayari kumuunga mkono mgombea wa UKAWA ambaye atapitishwa ikiwa si wewe.
Huku UKAWA hakuna kususia, kuna kushirikiana na kupambana tu”.
Aliandika J. Mtatiro kupitia ukurasa wake huo qa facebook.
Duru
mbalimbali za kisiasa zinaeleza kuwa, Kada huyo wa CCM, ambaye pia
alikuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, mapema leo aliita wanahabari
nyumbani kwake, Segerea na kutangaza rasmi kujiondoa CCM kwa kile
alichoeleza kubinywa kwa demokrasia ndani ya chama hicho hivyo ameamua
kuhama rasmi chama hicho.
Dk. Makongoro Mahanga akitangaza rasmi kukihama CCM, mapema leo nyumbani kwake, Segerea
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena