BAJETI ya Wizara ya Elimu, Sayansi,Teknolojia na Ufundi, juzi ilipitishwa kwa namna ya kipekee tofauti na ilivyozoeleka.
Hali hiyo inatokana na wabunge wa vyama
vyote, kuungana na kumtetea Waziri wake, Profesa Joyce Ndalichako,
wakitaka apewe muda aboreshe elimu.Wabunge
wamepitisha bajeti ya Sh trilioni 1.3 huku wakisisitiza serikali
iboreshe elimu nchini, ikiwa ni pamoja na kuondoa changamoto mbalimbali.
Wakati Bunge likiwa limekaa kama
kamati, ambako wabunge hushika mshahara wa waziri hadi wapate majibu ya
kuridhisha, kwa upande wa wizara hii, waziri husika alitetewa na baadhi
ya wabunge wakiwemo wa upinzani.
Mbunge wa Vunjo, James Mbatia
(NCCR-Mageuzi ) alilalamikia tatizo la vitabu shuleni, ikiwemo kukosewa
kwa mitaala, jambo alilotaka waziri kuzungumzia.
Akijibu suala hilo, Ndalichako alisema
nyaraka alizonazo mbunge yeye hana, hivyo aliomba kupatiwa afanyie kazi,
lakini Mbatia alikataa na kusema nyaraka hizo si za siri, kwani zipo
kwenye mitandao ya elimu huku kukiwa na vitabu vinavyotumika shuleni.
Baada ya mjadala wa muda mrefu, Mbunge
wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Maendeleo) aliingilia suala hilo na
kusema matatizo ya mitaala ni mapana.
Alishauri suala hilo lirudishwe kwenye
Kamati ya Bunge inayoshughulikia suala hilo kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Mbatia alikubaliana na ushauri wa Zitto na kurejesha shilingi, kisha
kuendelea na mjadala mwingine.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena