MARTHA MAGAWA
Imekuwa kawaida leo hii kwa wanaume walio wengi kuwa na nyumba
ndogo, hii yote ni katika kutafuta mapenzi motomoto ambayo
yatampagawisha. Akina dada mlio wengi mmejisahau sana kwa wapenzi wenu
na kuwasababisha kutoka nje ya mahusiano.
Leo hii asilimia 75 ya watu duniani ni
wanawake na 25% pekee ni wanaume, kwa idadi hiyo wanawake ni mara tatu
ya wanaume hivyo kwenye kila wanawake 75, 25 tu ndio wanaoweza kuwa na
wanaume, idadi iliyobaki hawana wanaume wa kudumu; hivyo hutumia kila
mbinu kuweza kupata mwanaume ambaye atamliwaza kama wanawake wengine.
Hivyo yakupasa uwe na kila mbinu za kuweza kumfanya mpenzi wako
akukumbuke kila mara na kutoweza kutoka nje ya mahusiano.
USAFI WA MWILI
;- Kitu cha kwanza kukizingatia kabla ya yote lazima mwanamke uuweke
mwili wako safi kabla ya tendo. Hii ikiwemo na kuoga mwili mzima,
kusafisha sehemu zako za siri ikiwemo na mahala popote ambapo
pamefichika kwani sehemu hizo wanaume walio wengi na wanaojua mapenzi
hupenda kuzichezea sehemu kwa kuwa ndizo ambazo huhifadhi mihemko ya
mwanamke.
USAFI WA MAHALI PAKUFANYIA TENDO;- hakikisha
unasafisha chumba au mahali ambapo umepaanda kwa ajili ya kuja
kumliwaza mwenzi wako kabla hajafika eneo la tukio. Hii ikiwemo
kutandika kitanda vizuri kwa rangi za upendo (nyekundu) kama huna basi
jitahidi kupata rangi yeyote ambayo ni nzuri ila usiweke shuka jeusi
kwani rangi nyeusi ni rangi ya huzuni, pia kuweka manukato mazuri
ikiwemo maua, kama ni wakati wa usiku ni vizuri kuandaa mishumaa au taa
ya rangi.
VAA NGUO FUPI :- vaa
nguo fupi (nusu uchi), hii humfanya mwanaume kupata mihemko pindi
anapokuona, pia humuandaa kisaikolojia na kuufanya mwili wake kuwa
tayari pindi utakapohitajika.
Baadhi ya wanawake hupenda kuvaa nguo fupi watokapo na kuwaonesha
watu wengine sehemu zao muhimu lakini hawafanyi hivyo kwa wapenzi wao
pindi
wawapo ndani, hii sio tabia nzuri muonesho mumeo kwamba hakubahatisha
kukuchangua wewe. Hakikisha nguo zako za ndani (chupi na sidiria)
ni safi na zenye mvuto.
USIMUUDHI MPENZI WAKO
:- hakikisha kwamba husababishi maudhi ya aina yeyote kwa mpenzi wako,
ikiwemo lugha chafu, kumzungumzia na kumsifia mwanaume mwengine, mpambe
mpenzi wako kwa majina mazuri (Babe, Honey, Sweetheart) na mengineyo
kama hayo kabla ya tendo. Baadhi ya wanawake huwaita waume zao majina
mazuri wakati wanapopewa zawadi tu au wakati wanapofikishwa kileleni hii
sio sawa kabisa, sababu huu utakuwa ni unafiki mwanaume aweze
kukufikisha kileleni anahitaji maandalizi bibi eeh.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena