Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MICHEZO ~ Tanzania yaitumbua Burundi ya Mavugo

Baada ya ushindi wa kwanza wa kocha Salum Mayanga akiifundisha Taifa Stars kama kocha mkuu wa muda na kufanikiwa kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Botswana Jumamosi ya March 25, leo March 28 2017 walicheza mchezo wao wa pili wa kirafiki wa FIFA dhidi ya timu ya taifa ya Burundi.
Mchezo dhidi ya Burundi ni mchezo ambao Taifa Stars ilikuwa ina mkosa nahodha wao Mbwana Samatta ambaye amerudi Ubelgiji kuungana na timu yake ya KRC Genk kujiandaa na mchezo wa robo fainali ya UEFA Europa League watacheza dhidi ya Celta Vigo ya Hispania.
Hata hivyo Taifa Stars ambayo ipo nafasi ya 157 katika viwango vya FIFA ukilinganisha na Burundi waliyo nafasi ya 139, wamefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1, magoli yakifungwa na Simon Msuva dakika ya 22, Mbaraka Abeid dakika ya 78 wakati goli pekee la Burundi lilifungwa na Laudit Mavugo dakika ya 54.
Taifa Stars sasa inakuwa imepata ushindi wa pili baada ya saa 48 toka ipate ushindi wa kwanza Jumamosi ya March 25, kwa mwaka 2017 pekee Taifa Stars inakuwa imecheza jumla ya mechi mbili na imepata ushindi mechi zote, kuzinfunga Botswana na Burundi waliyokuwa juu yetu katika viwango vya FIFA itasaidia Tanzania kusogea katika viwango hivyo.

Post a Comment

0 Comments