Uongozi wa Klabu ya Simba umeweka wazi mipango yao katika Dirisha la Usajili ambapo kwa Mujibu wa Makamu Rais wa Klabu hiyo Geofrey Nyange Kaburu, Simba haina mpango wowote wa kumuacha mchezaji.
Nyange amesema kwa kuwa wachezaji waliopo wameipatia Mafanikio Simba katika Msimu uliopita, hivyo hawaoni sababu kuwaacha badala yake yawapasa kutafuta nguvu kidogo na si kuwaacha wachezaji.
-Klabu haina Mpango wa kumuacha Mchezaji yoyote, tumeridhika na kazi yao, tutakachofanya ni kuongeza Nguvu kidogo katika kipindi hiki cha Usajili na si kubadilisha kikosi Kizima' Alisema Kaburu.
Kuondoka kwa Banda.
Akielezea kuhusu tetesi za kuondoka kwa Wachezaji Jonas Mude, Abdi Banda na Ibrahim Ajib, Makamu huyo wa Urasi wa Simba amesema hawaendi popote kwani tayari wamekwishakubaliana kusaini mkataba mpya.
-Tunataka kuwa na kikosi cha Muda mrefu, tayari tushazungumza nao na mikataba ipo tayari, bado kusainiwa tu kwani tumekamilisha kila hitaji lao, ni vijana ambao tumewalea sisi wenye hivyo tunaamini wataitikia wito wetu" Kaburu alifafanua.
Simba watakuwa wawakilisha wa Taifa Mwakani katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika, ambapo wachambuzi wa mambo wanashauri kikosi hicho kujijenga zaidi kwa kufanya usajili mzuri pamoja na kuwalinda nyota wao wasiende popote ili kuwa imara zaidi.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena