Akizungumza na wanakijiji cha utegi Afisa ardhi wa wilaya ya Rorya, ndg Fredy Kyalawa kwa niaba ya mkurugenzi aliwaambia wanakijiji cha Utegi umuhimu wa kupima viwanja vyao na faida ya kuwa na hati miliki ya kiwanja, aliwaambia wananchi kwamba kwa sasa waziri wa ardhi alitoa ofa ya punguzo kwa wananchi wa mkoa wa Mara, Akijibu maswali yaliyo ulizwa na wananchi alisema kipindi cha nyuma kupima kiwanja kimoja ilikuwa zaidi ya tsh milioni moja na zaidi kwa kiwanja kimoja, na kwamba kwa sasa garama za upimaji ni sh laki moja kwa kiwanja kimoja.
Akawataka wananchi wa mji wa Utegi kujitokeza angalau watu 50 ili kuweza kumudu garama za upimaji ili kuweza kuwaleta wataalamu na shughuli za kupima kuweza kuanza mapema na wenye viwanja kuweza kuandaliwa Hati miliki za viwanja vilivyo pimwa.
Mh diwani Peter Osoro Sarungi aliwataka wananchi kulipokea jambo hili la kupima viwanja vyao kwa mikono miwili ili kuwawezesha kuweza kukopesheka katika makampuni na taasisi za kibenki baada ya kupata hati miliki za viwanja vyao.
Katika mkutano huo walichaguliwa wajumbe 5 watakao hamasisha na kusimamia michango ya wananchi ambao watakuwa tayari viwanja vyao kupimwa. Mh diwani Sarungi amesema mji wa utegi ni mji ambao kiuhalisia unapaswa kupimwa na kuwa katika utaratibu wa mji ambao ni wa kisasa. Kwa sasa ujenzi unao endelea kiholela na watu kuuza maeneo bila utaratibu itakuja kuwa hasara kwani upimaji utakapofanyika utakujakuwa na hasara kwa wengine.
Pia amewataka Wananchi wa Utegi waishio nje na wana viwanja vyao wajitokeze kushiriki katika zoezi hili.
Picha na Kituo cha Habari na Mawasiliano Rorya.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena