Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | Utata Wa Kifo cha Jenerali Imran Kombe (Nani Anahusika?) Sehemu ya Kwanza


Related image
Jenerali kombe alikuwa ni mwanajeshi na kiongozi jushaa [hodari] wa nchi yetu na hasa alijulikana pale nchi yetu ilipoingia katika mapambano ya kurudisha ardhi yetu iliyochukuliwa na dikteta IDD AMIN DADA, kwani yeye ni moja wa makanda waliopambana mstari wa mbele katika vita ya kagera.

Unaweza kujiuliza kuhusu hiyo nick name aliyokuwa anafahamika nayo katika medani za kivita, alipewa hilo jina katika vita ya kagera kutokana na yeye kukusanya vikosi vyake na kuingia Uganda kwa kuvuka mto mkorofi ambao huu mto pia unajulikana kwa jina la mto mkorofi wa ngono[sababu kuu ya huu mto kuitwa hivi ni kuwa inaaminika mtu wa kwanza kuwa na virusi vya ukimwi duniani aliishi kando ya huu mto na inajulikana ulimwenguni kote kuwa njia kuu ya kuambukizwa ukimwi ni kufanya ngono]. Baada ya kuisha kwa ile vita jenerali kombe alipandishwa cheo na kuwa mnadhimu mkuu wa jeshi [CHIEF OF STAFF] ambacho alikitumikia kwa muda Fulani, na ilipofika kipindi cha utawala wa DR. ALI HASSAN MWINYI jenerali kombe aliteuliwa na kuwa mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa.

Katikati ya mwezi wa june mwaka 1996 jenerali kombe alivuliwa wadhifa aliokuwa nINAENDELEAenzi wa usalama wa taifa] na hii ilikuwa ni kipindi cha mwanzo kabisa cha utawala wa mheshimiwa BENJAMNI WILLIAM MKAPA kwani huyu raisi aliingia madarakani mwaka 1995. Kwahiyo baada ya kuvuliwa wadhifa wake akabaki kuwa mstaafu lakini kwa mujibu wa sheria alikuwa anapewa ulinzi na mahitaji mengine kama wastaafu wengine wa nyadhifa za juu serikalini na jeshini.

MAUAJI YA JENERALI KOMBE 
Mwaka 1996 gari aina ya NISSAN PATROL iliibiwa jijini DAR ES SALAAM na mwizi maarufu wa magari wa kipindi hicho aliyekuwa akijulikana sana kwa jina moja la WHITE [nimekosa jina lake halisi kwani hakuna chanzo kilichotaja au kujua jina lake halisi], gari hilo lilikuwa limesajiliwa na namba za usajili [TZD 8592] na lilikuwa mali ya mfanyabiashara W. LADWA.

Baada ya jeshi la polisi kupata taarifa za uwizi huo walianza kufanya uchunguzi kujua na kubaini ni yuleyule mwizi sugu wa magari maarufu kwa jina la WHITE. ndipo hapo mkuu wa jeshi la polisi kanda maalumu ya DAR ES SALAAM aliamuru askari wawili kwa majina ya koplo JUMA MSWA na konstebo MATABA MATIKU wakiwa na silaha aina ya PISTOL CHINESE-TYPE kwenda katika mkoani KILIMANJARO, MOSHI.

Kamanda wa DAR ES SALAAM aliamuru hivyo waende moshi kwasababu walipata taarifa kuwa jambazi WHITE yuko kati ya ARUSHA na MOSHI, wale askari wawili walivyofika moshi walipokelewa na kamanda wa Kilimanjaro huku nyuma tayari kamanda wa DAR alikuwa ameshawasiliana na kamanda wa KILIMANJARO kuwa kuna vijana wangu nimewatuma kazi huko ya kutafuta gari lilioibiwa DAR.

Kamanda wa moshi alitoa askari wake watatu na kuungana na wale wawili wa kutoka DAR, hawa askari watatu wa MOSHI walikuwa na bunduki aina ya MACHINE GUN na wakaanza msako mara moja wa kutafuta wapi gari lilipo pamoja na jambazi WHITE na ikumbukwe kipindi hicho gari aina ya NISSAN PATROL ilikuwa ni gari ya kifahari sana na zilikuwa chache sana.

Mnamo tarehe 30 juni 1996 wale askari watano wakiwa katika gari yao ya polisi katika randa randa zao za kutafuta gari iliyoibiwa, gafla waliona gari aina ya Nissan patrol amabayo ilikuwa ikifanana na ile iliyoibiwa DAR hapohapo wakaanza kuifukuzia kwa nyuma huku wakiipiga risasi, takribani risasi kumi na nne zilipigwa kwenye ile Nissan waliokuwa wanaifukuzia wale askari.

Katika zile risasi zilizopigwa kuna risasi zililenga tairi na hivyo kupelekea gari la jenerali kombe kuanza kuserereka na mwishoe likaegemea mahali na kusimama, kwa bahati mbaya sana siku hiyo jenerali kombe hakutembea na walinzi wala dereva wake, yani alikuwa yeye na mke wake ROSSELEEN tu. Na ndo maana jenerali alihofia kusimamisha gari kwani alihisi labda wale majambazi wanataka lumuibia au wametumwa kumuua na ikumbukwe huyu alikuwa mkurugenzi wa usalama wa taifa kwahiyo watu kama hawa mara nyingi ni MOST WANTED.

Huku nyuma askari wale wakaona gari limesimama na hatimaye tu walivyofika wakashuka haraka huku wote wakiwa wameshika bunduki zao [nimeshaelezea kila mtu alikuwa na aina gani ya silaha], wakati askari wanakaribia kuwafikia jenerali kombe na mkewe huku nyuma tayari jenerali alikuwa ameshatoka ndani ya gari yake. 
Alipokuwa ametoka ndani ya gari alikuwa karibu kabisa na gari yake huku akitahamaki haelewi ni nini kinaendelea.

Wakati jenerali anatahamaki wale askari wakawa wameshafika eneo la tukio huku nyuma mke wa jenerali naye alikuwa ameshuka upande wa pili wa mlango wa mbele, wale askari walipomkaribia tu jenerali wakamyooshea bunduki huku wakijatambulisha sisi ni askari na kati yao kulikuwa na wngine wamevaa sare, jenerali kombe kutokana na kuwa na uzoefu na mambo ya kiusalama hakutaka kuonesha makuu kuwa yeye alikuwa ni nani katika usalama wa nchi na jeshini…

Kwa haraka kabisa jenerali kombe aliinua mikono juu kuonesha wale askari kuwa ametii agizo ingawa bado alikuwa anatahamaki ni vipi tena naoneshewa bunduku na vijana[askari] ambao walikuwa chini yangu juzi tu hapa kabla sijastaafishwa, cha kushangaza wale askari wawili kutoka DAR wakamiminia jenerali kombe risasi nne kifuani mwake bila kuwa na huruma wala kujali kuwa jenerali amesalimu amri kwa kunyoosha mikono juu.

Jenerali kombe alijeruhiwa vibaya sana na zile risasi zilizompata kifuani na hatimaye akapoteza maisha papo hapo, mkewe alizunguka mbele ya gari na kwenda pale chini alipoanguka mumewe na kuanza kumshika huku akilia sana kwa uchungu na kusema “mnajua nani mliyemuua….?” Wale askari hawakutaka kusikiliza chochote, wao walichofanya ni kuwachukua wote na kwenda kuwapeleka sehemu husika ambapo mumewe alipelekwa hospitalini na mkewe alipelekwa kituoni kwa ajili ya mahojiano.

Kule kituoni mke wa jenerali alitoa maelezo kuwa yeye ni nani na aliyeuwawa ni nani, baada ya maelezo hayo kamanda wa polisi Kilimanjaro akapewa taarifa kuwa Yule aliyepigwa risasi alikuwa ni jenerali kombe ndipo yeye akawasiliana na kamanda wa Dar na kumjulisha kilichojiri naye kamanda wa Dar akaongea na mkubwa wake ambaye ni mkuu wa mapolisi Tanzania[IGP]. Baada ya maelezo yake, mke wa jenerali kombe akaachiwa na kwenda hospitalini aliko mumewe na vyombo vya habari huku nyuma vya Tanzania na vya nje ya nchi vikaanza kuripoti tukio lililotokea na nchi nzima ilipatwa na simanzi kutokana na msiba huu mkubwa wa kiongozi shujaa wa vita ya kagera.
Itaendelea sta Tuned

Post a Comment

0 Comments