Header Ads Widget

Responsive Advertisement

FAHAMU | Utata Wa Kifo cha Jenerali Imran Kombe (Nani Anahusika?) Sehemu ya Pili ( Finale)

Image result for Tanzania High Court
Mkuu wa mapolisi akaagiza uchunguzi uanze na pia wale maaskari wote watano watiwe nguvuni mara moja, na kweli lile agizo lilitekelezwa kwa wale vijana kushikiliwa mahabusu kwa ajili ya mahojiano na kuruhusu uchunguzi uendelee pamoja na sababu za kiusalama.

Baada ya uchunguzi kukamilka wale askari walifikishwa mahakamani na kushtakiwa kuua kwa kukusudia na kesi yao ikaanza kusikilizwa huku wengi wa watu wakisikilizia maamuzi ya mahakama kwani hata mataifa ya nje nayo yalikuwa yanasubiria hatima ya hii kesi huku wakilaani kitendo kilichotokea ni cha kinyama na uzembe uliopitiliza kwani ilikuwa imeshatia doa jeshi la polisi na serikali nzima ya wakati huo.

Baada ya miaka kadhaa ya kusikilizwa kesi, mnamo mwaka 1998 mahakama kuu ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ilitoa hukumu kwa washtakiwa waliomuua jenerali kombe kunyonwa mpaka wafe kwani mahakama ilisema imebaini kuwa washtakiwa wamemuua jenerali kombe kwa makusudi kabisa na sio bahati mbaya kama wao walivyodai mbele ya mahakama.

Ikumbukwe kuwa kati ya wale askari watano ni askari wawili ndo waliopatikana na hatia ya mauaji na ni wale askari kutoka DAR na ndo waliohukumiwa kunyongwa na mahakama kuu, wale askari wengine walionekana kuwa hawana hatia na kuachiwa huru kwasababu hawakuhusika moja kwa moja na mauaji ya jenerali kombe.

Baada ya ile hukumu wengi walisifia huo uamuzi wa mahakama kuu kuonesha haki bila upendeleo na wale askari wakapelekwa gerezani kusubiria raisi mkapa kutia saini ya kuhidhinisha kuwa wanyongwe [kwa mujibu wa sheria za nchi yetu raisi ndo mtu pekee mwenye mamlaka ya kuhidhinisha kwa kutia saini ya watu Fulani kunyongwa]. UTATA ULIOPO KATIKA MAUAJI YA JENERALI KOMBE

UTATA NAMBA MOJA [1]- Jenerali kombe alipovamiwa na wale askari na yeye baada ya kugundua kuwa wale ni askari na sio majambazi kama alivyohisi mwanzo alinyanyua mikono juu kuonyesha hali ya kusalimu amri kwani tayari alikuwa ameshaonyeshwa bunduki na pia jenerali kombe hakuwa na silaha yoyote na hakuonesha dalili yoyote ya kutotii amri lakini cha ajabu walimchapa risasi bila huruma.

UTATA NAMBA MBILI [2]

UTATA NAMBA MBILI [2]- Hivi inawezekana vipi wale askari kuwa hawamjui jenerali kombe ambaye kipindi cha nyuma tu hapo alikuwa ni boss wao, kweli…??? kabisa wanamuona sura yake halafu wanasema kuwa walimfananisha na yule jambazi WHITE, na pia huyu jenerali alikuwa maarufu kutokana na ile vita ya kagera lakini bado walikuwa hawamjui eti, mmmmh....!!!! yani ulikuwa ni uwongo uliotukuka na ndo maana mahakama walisema hawa wameua kwa kukusudia.

UTATA NAMBA TATU [3]- kwa inavyofahamika kisheria kabisa kuwa mtuhumiwa anapokubali kusalimu amri na tena kwa kunyoosha mikono juu huruhusiwi askari kumpiga risasi na tena ukiangalia uwiano ulipo kati ya mtuhumiwa na askari waliopo, mtuhumiwa mmoja askari watano halafu unampiga risasi kweli…..? acha hiyo na pia ikumbukwe kuwa jenerali kombe hakuwa na silaha siku hiyo, sawa basi ni kwanini usimpige mguuni ambako ndo sheria inataka kwa mtuhumiwa mbishi, ila wao kuonyesha walidhamiria walimlenga kifuani. Kwani kumlenga mtuhumiwa kifuani au kichwani basi wewe umedhamiria kwa dhati kwani hizo ndo target ambazo ukipigiwa asilimia zaidi ya 95 lazima ufe papo hapo.

UTATA NAMBA NNE [4]- Hawa wauaji baada ya ile hukumu ya kunyongwa, walikaa gerezani kwa miaka kadhaa na serikali ya kipindi hicho ikawapunguzia kutoka hukumu ya kunyongwa mpaka hukumu ya kifungo cha maisha (hii ni kwasababu raisi aliyekuwa madarakani wakati huo alikataa kusaini ili wawezwe kunyongwa), hii inaonesha walionewa huruma na kusahulika kuwa hawa walikuwa ni wauaji ambao mahakama kuu yenyewe iliwachukulia askari hawa kama wauaji waliokusudia… haya tuache hayo.

Tujikumbushe kidogo maamuzi magumu yaliyofanywa na raisi nyerere pamoja na mwinyi walivyoweza kusaini watu wanyongwe na walikuwa wanajulikana kwa huruma walizokuwa nazo katika uongozi wao ila ilibidi wasaini kwasababu ya umuhimu wa watu waliouwawa. Mfano mwalimu Nyerere aliidhinisha kunyongwa kwa ABDALLAH MWAMINDI aliyemuua DK. WILBERTN KLERUU aliyekuwaga mkuu wa mkoa wa IRINGA, mfano kwa raisi ali Hassan mwinyi yeye aliidhinisha kunyongwa kwa kanali wa jeshi la wananchi [JWTZ] ambayeb alipatikana na hatia ya mauaji ya kutisha.

Muuendelezo wa UTATA NAMABA (4), Kwa hiyo mifano miwili inawezakana vipi raisi aliyekuwa madarakani kipindi hicho kushindwa kuiidhinisha wale askari wanyongwe kwani walikuwa wamemuua jemedari alyekubali kufa kwa ajili ya nchi [vita ya kagera] na pia alikuwa mkurugenzi katika sekta nyeti sana nchini ambayo inategemea kubaini watu wabaya.

Cha kushangaza kupitiliza hawa wauaji baada ya raisi kikwete kuingia madarakani, mnamo mwaka 2011 waliachiwa huru, yani kutoka kunyongwa kwenda kifungo cha maisha kwenda kuwa huru, hii iliamsha hisia upya kwa wapenda haki walihoji kuwa inawezekana vipi hawa wauaji wanaachiwa huru…? Ila ndo hivyo imekuwa ZILIPENDWA…..!!!! UTATA NAMBA TANO [5]- Baada ya hawa wauaji kuachiwa huru vyombo vya habari na taasisi mbalimbali zilihoji sana kuachiwa huru kwa hawa wauaji, ndipo watu wakahoji ni nani aliyetoa msamaha kwa hawa wauaji kuachiwa……? Hilo swali ni gumu mpaka leo kwani halina jibu lake…

Kwani kila aliyeulizwa anasema sio mimi niliyetoa ruhusa, na tarehe 13 oktoba 2011 kupitia mkurugenzi wa mawasiliano ikulu raisi kikwete alitoa chapisho kuwa sio yeye aliyetoa msamaha kama gazeti la mwananchi lilivyokuwa likimtaja kuwa yeye ndo aliyetoa msamaha kwa wauaji hao na kudai hayo maamuzi yalifanywa kabla yeye hajaingia madarakani tarehe 21 disemba 2005 na hakuna yoyote aliyekubali kuwa yeye ndo alitoa amri ya wauaji hawa kuachiwa mpaka Leo hii.

WASHTUMIWA WA TUKIO LA MAUAJI NJE YA WALE ASKARI

Kumekuwepo na kushtumiwa kwa watu tofauti ukitoa wale maasakari waliohusika, [1]- serikali iliyoko madarakani kipindi hicho wengi waliishtumu kuhusika moja kwa moja na tukio lile kwani inasemekana jenerali kombe alikuwa akivujisha siri kwa mpinzani wa kipindi hicho LYATONGA MREMA na hii haikufurahishwa na serikali iliyopo na pia alikuwa akiwaingilia vigogo wa juu katika mambo yao. [2]- mshtumiwa huyu alihusishwa na mauaji ya jenerali ni baada ya ripoti kutolewa na CIA ya marekani kuwa raisi wa Rwanda bwana kagame alihusika moja kwa moja na mpango mzima wa mauaji ya jenerali, unaweza kwenda kusoma mwenyewe vizuri hiyo ripoti kupitia tovuti yao kwani ni ndefu siwezi kuielezea yote ila kwa ufupi ni hivyo

Watu wengi walichotegemea raisi kikwete angefanya kabla hajatoka madarakani ni, 
CHA KWANZA (1), kukana kutotoa msamaha [hiyo tayari alifanya] na kuwarejesha wale wauaji gerezani na kuendelea kutumikia kifungo cha maisha au kunyongwa kwasababu kuachiwa kwa hawa wauaji ni kinyume na katiba na sheria za nchi yetu. 
CHA PILI (2), angeweza kukiri kutoa msamaha kwa wauaji wale kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu kwa ibara ya 45 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa mara kwa mara. Ila haikuwa hvyo kwani kwa sasa tuko kwenye uongozi mpya wa DR. JOHN POMBE MAGUFULI, labda raisi wetu wa sasa ataweza kukata kiu yetu ya kutendewa haki kwa jemedari wetu IMRAN KOMBE.

Napenda kumalizia kwa kuwapa pole familia yote ya kombe, na kuwasihi waendele kufuatilia haki zao ikiwemo ile fidia iliyoidhinishwa na mahakama kuu kulipwa tajribani milioni 600 na nilipata taarifa kuwa tayari ameshalipwa milioni 300 ingawa kwa usumbufu mkubwa na upotezwaji wa muda wake mkewe, tutamkumba daima hayati jenerali IMRAN KOMBE kwa ushajaa alionyesha katika vita ya kagera kwa kukubali kufa kwa ajili ya taifa letu…. Kweli alikuwa shujaa wetu, mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi…. AMINA…!!!! MWISHO....!!!!

Post a Comment

0 Comments