Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Fahamu | Wizi Mkubwa Wa Benki Ulioshirikisha Wataalamu Kuwahi Kutokea Duniani : Episode 1.

Image result for bank robbery in fortaleza
Bank Kuu ya Brazil

Uwizi wa uvunjaji wa benki umekuwa ni aina ya uwizi upendao sana na wezi kutokana na benki ndo nyumbani kwa fedha, kwani baada ya serikali nyingi duniani kuweka mifumo inayolazimisha watu kuhifadhi fedha zao benki, kwa mfano mishahara kupitia benki, malipo ya bili tofauti kupitia benki N.K na hii hali ndo imefanya fedha kukauka majumbani na kupunguza uvunjaji wa manyumba ya watu kwani sasa kila mwizi anajua fedha ziko benki na ndo wezi nao wanazifuata hukohuko. Kutokana na maelezo hayo leo tutaenda kuona uwizi unaoshika rekodi namba moja kwa kiasi kikubwa cha fedha kuibiwa ndani ya benki.

Sababu nyingine inayopelekea huu uwizi kuwa Maarufu zaidi duniani ni kutokana na kuwa uwizi namba moja duniani uliohusisha wasomi (wataalamu) wa hali ya juu, kwani wezi waliohusika walikuwa na elimu na uzoefu wa juu wa taalamu zao. Wezi wote waliohusika walikuwa wana elimu ya MASTERS na PHD (wasomi wezi). Na pia uwizi huu ulifanyika benki kuu ya nchi (ingekuwa Tanzania tungesema wameiba BOT pale posta) na unafahamu vizuri ulinzi wa benki kuu unavyokuwaga na mkali kwani ndo fedha za nchi zinapohifadhiwa ila wanyama walifanya yao na kufanikiwa kwa kutumia taaluma, ufundi na ustadi wa hali ya juu.

Mwaka 2005 katika nchi ya Brazil mji wa FORTALEZA kulitokea tukio la kihistoria katika nchi hiyo ambayo haitasahaulika na itakuwa simulizi itakayohadithiwa vizazi na vizazi kwa utaalamu na ufundi wa hali ya juu uliopangika kisomi kuliko kawaida.

Wezi katika ubora wao na kutumia vizuri taaluma zao kuhakikisha wanastaajabisha dunia kwa kufanya tukio lililokuja kuingia katika kitabu cha rekodi za dunia [GUINESS WORLD RECORD], na siku zote ukiona tukio lako limeingia kwenye hiki kitabu ina maana hilo sio tukio la kawaida machoni mwa watu.

MIPANGO YA TUKIO

Hili tukio lilipangwa kwa ustadi mkubwa mno kwani lilihusisha wasomi wa fani mbalimbali katika upangaji hadi kufanikisha tukio zima. Ni tukio la aina yake kwani uwizi ulifanyika katika BENKI KUU YA BRAZIL [namaanisha kama unavyosema BOT hapa Tanzania] katika mji wa FORTALEZA.
Image result for LUIS FERNANDO RIBEIRO

Kuna jamaa mmoja maarufu sana nchini BRAZIL kwa biashara ya madawa ya kulevya anajulikana kwa jina la LUIS FERNANDO RIBEIRO, huyu RIBEIRO ndo mhusika mkuu wa tukio zima [mastermind] kwa kuratibu kila kilichohitajika katika tukio zima.

Bwana RIBEIRO ni mtu mwenye pesa, sema ni pesa chafu kutokana na madili yake mengi anayofanya sio halali, ndipo aliamua kupanga kufanya tukio la kihistoria lililoacha alama kubwa katika taifa la BRAZIL.

MPANGO ULIKUWA HIVI, bwana Ribeiro alikusanya vijana wapatao 24 wenye taaluma tofauti zikiwemo wanamahesabu, wahandisi, wajiolojia na wafanyakazi wa zamani wa benki kuu [kwa mujibu wa ripoti hawa walikuwa ni wafanyakazi waliofukuzwa kwa makosa ya rushwa na uwizi] ambao hawa watu walikuwa tayari kufanya hili tukio na haikuwa kazi ngumu kwake kwani anajua wezi wengi na wasifu wao katika nchi ya brazil.

Baada ya kumaliza kazi ya kukusanya vijana wake aliwapa mawazo yake ni namna gani watavamii benki kuu na wale vijana nao waliongezea mawazo yao ili kuweza kufanikisha jambo lao na walitumia siku nne mfululizo kujadiliana ni namna gani watavamia, yani wote 25 ikiwemo RIBEIRO walikaa kambi kujadiliana.

Baada ya majadiliano ya siku nne ndo wakaja na mpango uliokamilika A-Z na huo mpango ulikuwa hivi, 
CHA KWANZA, wafungue kampuni ya kuzuga kuwa wanafanya biashara Fulani ili waweze kwanza kuwaharibu kisaikolojia watu watakao kuwa wamewazunguka pamoja na jeshi la polisi, swali linakuja biashara gani…..? katika majadiliano yao walikuja na wazo la biashara ya kuuza nyasi za asili na bandia pamoja na mimea kwa ujumla, kwahiyo itakuwa inaitwaa kampuni ya mandhari[landscaping]. Unaweza kujiuliza kwanini walichagua biashara hiyo…? Ni kwasababu hii biashara inawapa mwanya wa kuweza kuchimba na hata wakiwa wanatoa michanga nje hakuna wa kuwahoji kwani wanajulikana wanafanya biashara inayohusiana na mambo ya kuchimba mchanga kwa ajili ya upandaji wa nyasi na mimea kwa ajili ya kuwauzia watu.

CHA PILI, kuhakikisha wanatafuta eneo, nyumba au jengo lililo karibu na benki kuu ili kurahisisha kazi yao, kwahiyo walianza kazi ya kutafuta... Hiyo picha hapo juu ndo LUIS FERNANDO RIBEIRO. 

CHA PILI, kuhakikisha wanatafuta eneo, nyumba au jengo lililo karibu na benki kuu ili kurahidisha kazi yao, kwahiyo walianza kazi ya kutafuta na mwishoe wakapata nyumba iliyokaribu ambayo walimvua mtu kwa kumlaghai mwenye nyumba kwa kumpa kiasi kikubwa kuliko bei ya nyumba na hivyo mwenye nyumba akamtoa aliyekuwepo na kuwakodishia hawa wezi bila kufahamu.

CHA TATU, ni kupata ramani ya chini ya ardhi ya mji mzima wa FORTALEZA, unaweza kujiuliza ni ya nini hiyo….? Umuhimu wake ni kuwa kama tunavyojua chini ya ardhi huwa kunapitaga mabomba ya aina nyingi kama ya maji, mafuta, gesi na maji taka, sasa ukichimba bila ramani unaweza kujikuta umekata moja ya haya mabomba na itakuwa mpango umeshaingia dosari na ikumbukwe kuwa hawa wezi walichimba kwa vifaa vya kisasa ambavyo ukijisahau unajikuta umeshakata bomba, na hii kazi ya kuja na ramani waliachiwa wanajiolojia na walitekeleza vizuri tu.

CHA NNE, ni kujua je udongo wa eneo wanaloenda ni wa aina gani, hili lilikuwa rahisi kwani lilikabidhiwa kwa wahandisi na walileta jibu mapema tu kuwa maeneo yote ya karibu na benkii kuu udongo wake ni kichanga, kihivyo hautatusumbua katika kuchimba.

CHA TANO, ni kengele ya tahadhari ni namna gani wataiweza kuizuia isifanye kazi, hili jukumu walipewa wafanyakazi wa zamani wa benki nao wakalifanyia kazi na kuja na majibu yake ambayo tutakuja kuona huko mbele ya simulizi yetu.

Baada ya kila kitu kukamilika, hawa wezi katika majadiliano yao walikubaliana kazi itaanza mwanzo kabisa wa mwezi mei, kwahiyo mwezi mei ulivyofika walikodisha nyumba mojawapo karibu na benki kuu ile waliyomvua mtu ambayo hii nyumba ilikuwa namba 1071 katika mtaa wa MARCO katika mji wa Fortazela.

Baada ya kuipata hiyo nyumba wakanza kuifanyia maboresho ili iwe katika mazingira kweli ya kufanyia biashara ya nyasi na mimea kwa ujumla. Kazi ya uboreshaji ilipoisha wakaweka bango linalotoa ishara kuwa wao ni kampuni ya inayojihusisha na uuzaji wa nyasi asili na bandia, kwahiyo kila aliyeona bango alijua kuna muwekezaji anafanya biashara ya kuliingiza pato nchi kumbe sivyo.


Itaendelea...Tukutane Hapa Hapa.......
Credits | Mitandao

Post a Comment

0 Comments