John Dillinger |
Jina maarufu zaidi alilojipatia alijiita George Nelson, almaarufu kama baby face Nelson kutokana na muonekano wake wa kitoto, kisura na umbile. Hata hivyo ilikua si rahisi mtu kumuita baby face mbele yake na mara nyingi wenzie walimuita Jimmy.
Huyu baby face Nelson alikua ni jambazi wa kupora mabenki kipindi cha miaka ya 1930, akishirikiana kwa ukaribu na jambazi mwingine maaraufu sana John Dillinger (mhalifu wa kwanza kuwa adui namba moja wa umma/jamii) public enemy.
Baby Face |
FBI hao ni Herman Hollis, Samuel P. Cowley na W. Carter Baum.
Baby face Nelson alikua mtundu toka utoto wake kwani akiwa na miaka 7 tu aliwahi kukamatwa kwa kosa la kumpiga risasi kwa bahati mbaya mtoto mwenzie kwa kutumia pistol aliyokua ameikota hapo mtaani.
Akiwa na miaka 13 alijikuta mikononi mwa polisi tena kwa kosa la wizi, na akafungwa mwaka mmoja na nusu.
Akiwa bado kijana mdogo alipewa uongozi wa kikundi chao cha uhalifu.
Mwaka 1928 alimuoa Hellen Wawzynak na kujaaliwa kupata watoto 2.
Ndani ya miaka 2 baada ya ndoa yake Nelson na kundi lake walikua tayari wanajihusisha na uhalifu wa kupanga na uporaji wa mabenki.
January 6 1930 Nelson na wenzie walimvamia bwana Charles M. Richter nyumbani kwake, wakiisha kukata nyaya za mawasiliano ya simu ili kusiwepo mawasiliano, walimfunga na kumtesa bwana Charles aoneshe wapi pesa zilipo. Walifanikiwa kupata vito vya thamani kiasi cha dola 25,000 sawa na dola 360,000 kwa makadirio ya sasa.
Miezi 2 baadae walivamia tena sehemu nyingine na kupora vito vya thamani ya dola 50,000. Ni kipindi hicho vyombo vya habari viliwabatiza jina la the tape bandits .
April 21 1930 Nelson na wenzie walivamia na kupora bank ya kwanza, walifanikiwa kuondoka na kiasi cha dola 4,000 tu. Mwezi 1 baadae walivamia tena nyumba ya mtu na kupata vito vya thamani ya dola 25,000.
October 3 mwaka huo huo Nelson alipora benki ya pili na kupata dola 4,600. Mmoja wa wahudumu wa benki alimtambua kama mmoja wa waporaji, benki hiyo ilikua ni Itasca state Bank. Baada ya siku 3 Nelson alimpora mke wa meya wa Chicago, Big Bill Thompson vito vya thamani ya dola 18,000 za kimarekani.
Katika maelezo yake huyo mama alimuelezea Nelson kama kijana mwenye muonekano mzuri, na sura ya kitoto akisema nadhani ni bado kijana mdogo kabisa.
November 23 Nelson na kundi lake walihusishwa na wizi ambao hakufanikiwa katika nyumba moja huko Illinois tukio lililoacha watu 3 wamefariki na wengine kujeruhuwa. Baada ya siku tatu Nelson alivamia tavern moja huko Waukegan na kusababisha kifo cha mtu mmoja bwana Edwin R. Thompson baada ya kupigwa risasi na Nelson.
Mwaka 1931 sehemu kubwa ya kundi la Nelson walikamatwa na kufungwa akiwemo Nelson mwenyewe ambapo alihukumiwa kifungo cha mwaka 1 jela. Nelson alitoroka mwanzoni mwa mwaka 1932 katika msafara wa kahamishiwa wafungwa na kupewa hifadhi na mcheza kamari na bosi wa vikundi vya kihalifu bwana William Graham.
Nelson aliunda kikundi kipya cha uhalifu kwa kuwachukua waporaji wengine Homer Van Meter, Tommy Carroll, Eddie Green na wezi wengine 2 kisha wakavamia National Bank of Brainerd, Minnesota. Walifanikiwa kuondoka na kiasi cha dola 32,000 mnamo October 23, 1933. Mashuhuda wanaelezea kua Nelson alipiga risasi hovyo wakati wa kukimbia kutoka kwenye machine gun yake. Baada ya tukio alimchukua mkewe Hellen na mtoto wao wa miaka 4, pamoja na kundi lake wakaelekea San Antonio, Texas.
December 9, 1933 mwanamke mmoja aliwaambia polisi wa hapo San Antonio juu ya uwepo wa majambazi sugu eneo hilo. Siku mbili baadae Tommy Carroll alijikuta mtu kati baada ya kubanwa na wapelelezi 2, Tommy alifyatua risasi na kumuua papo hapo mpelelezi H.C Perrin na kumjeruhi mpelelezi Al Hartman. Kundi zima la Nelson lilitoroka San Antonio pamoja isipokua Nelson na mkewe wao walienda San Francisco na kumchukua John Paul Chase na Fatso Negri katika katika uporaji hapo San Francisco.
Mwaka 1934 Nelson na kundi lake waliendesha uporaji katika mabenki wakiongozwa na John Dillinger, mporaji mtukutu aliwahi kutoroka jela mara mbili, kwanza alitumia bastola ya mbao aliyoichonga mle gerezani kwa kumteka nayo askari, pili Nelson na wenzie waliwahi mtorosha kwa kulipua mabomu getini na kuingia na gari hadi eneo la gereza, pamoja na askari magereza kupambana kwa silaha lakini Nelson alifanikiwa kumtorosha Dillinger.
Mwaka huo huo 1934 ndio John Dillinger alikua adui namba moja wa jamii/umma. Yaani public enemy # 1.
July 22 1934, Dillinger aliuawa katika shambulizi la kushtukiziwa lililofanyika alipokua akitoka kuangalia muvi kwenye jumba la sinema la Biograph Theater baada ya mama mwenye nyumba wake alipokua kajificha kwa wiki kadhaa kuwajulisha FBI kwa makubaliano kuwa FBI watasaidia kuhakikisha yule mama harudishwi kwao kufuatia kukaa marekani bila kibali. Dillinger aliuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 4 huku moja ikimpata kisogoni na kutokea pembeni kidogo ya jicho.
Siku iliyofuata FBI walitangaza kua sasa pretty boy Floyd ndio public enemy # 1 kufuatia kifo cha dillinger.
October 22, 1934 pretty boy Floyd aliuawa katika mapambano na polisi pamoja na FBI hivyo kufanya bwana Baby Face Nelson kuwa public enemy # 1 sasa.
23 august mwaka huo huo Homer Van Meter aliawa na polisi huko st. Paul, Minnesota hivyo kufanya Nelson kuwa ndio mtu pekee aliebaki hai katika kundi lao.
Asubuhi ya November 27, 1934 Nelson, akiwa na mke wake pamoja na John Paul Chase wakiwa katika gari ya wizi Ford V8 walikuwa wakielekea Chicago, Nelson akiwa makini muda wote kuwatambua polisi au FBI waliokuwa wanamfuatilia aliiona sedan iliyokuwa inaelekea upande wanatokea wao. Sedan hiyo ilikua ikiendeshwa na jasusi wa FBI William Ryan akiwa na Thomas Mcdade.
Wote majasusi wa FBI na Nelson walitambuana kwa pamoja na baada ya kona za ghafla zile U-turn kadhaa kwa gari zote mbili kina Nelson walianza kuikimbiza gari ya FBI huku Nelson akiwa kaumia na risasi zikirindima kila kona, FBI walipata nafasi na kwenda spidi kisha wakawa wanangoja kina Nelson waje huku wao wakiwa tayari kabisa kuwashtukiza ( ambush) . Muda huo kina Nelson kama waliotea wakaacha kuwakimbiza.
Mcdade na Ryan hawakujua kumbe katikati ya mapambano risasi moja ilipasua pampu ya maji ya V8 ya Nelson hivyo kufanya ishindwe kwenda kwa spidi. Wakati huo Hudson automobile ikiendeshwa na FBI Herman Hollis ( moja ya waliopiga risasi zilizomuua John Dillinger July) pamoja na cowley walianza kuikimbiza V8 ya kina Nelson.
Huku Hollis na Cowley wakijaribu kuisimamisha gari ya kina Nelson, bwana Nelson alizungusha usukani, wakati huo aliekua akiendesha alikua mkewe Nelson ( Hellen) na kufanya gari ielekee upande wa Barrington Park na kusimama.
Gari ya FBI ilisimama umbali wa mita 30 hivi kutoka ilipokua gari ya kina Nelson huku FBI wakitumia gari yao kama ngao (cover). Mapambano yakaanza tena na kushuhudiwa na watu wengi waliokuwa wakipita karibu na eneo hilo.
Nelson alimuamuru Hellen ajifiche kwenye kijibonde kidogo huku yeye na Chase wakipambana na wale FBI na vita ya risasi ikaanza.
Katika mapambano risasi toka kwa Cowley ilimpata Nelson kwenye sehemu ya tumbo, ikapita kwenye ini, kisha kwenye kongosho na kutokea sehemu ya chini ya mgongo. Nelson akainama kwenye ile Ford V8, bila kutamka neno lolote lile akachukua bunduki toka kwa Chase na kumimina risasi zote kwenye gari la wale FBI.
Wakati risasi zikiendelea kurindima Nelson alilalamika kua Thompson machine gun yake ilikua inakwama, akaitupa na kuchukua 351 Winchester rifle ambayo ilikua imerekebishwa kupiga mfululizo ( fire fully automatic) .
Huku akiwa kajeruhiwa vibaya Nelson alitoka nyuma ya ile V8 na kuendelea kupiga risasi akitembea kuelekea ile gari ya wale FBI, risasi mbili toka kwenye Winchester ya Nelson zilimpata Cowley moja kifuani na moja tumboni na kupelekea Cowley kuanguka. Hollis alipiga risasi zilizompata Nelson miguuni na kuanguka pia.
Nelson akawa anainuka tena hapo Hollis akimbilia kwenye sehemu nyingine kujificha, Hollis akiwa anachomoa bastola yake alipigwa risasi ya kichwa na kujeruhika vibaya sana. Nelson akenda mpaka alipokua amelala Hollis akiwa hali mbaya, akasimama juu ya mwili ya Hollis huku Winchester yake inafuka moshi kisha kama mtu aliegutuka hivi akaiendea ile Hudson waliyokuja nayo wale FBI, akaendesha hadi ilipokua gari yao. Baada ya kupakia silaha zao na vitu vingine muhimu akamuamuru chase aendeshe kuondoka eneo hilo huku akiwaacha wale FBI taabani wahututi.
Wakiwa njiani kutoka eneo la tukio, Nelson alimwambia mkewe sasa nakufa, akamuelekeza chase aendeshe gari kuelekea kwenye nyumba yao ya maficho ( safe house) kwenye mtaa wa walnut huko wilmette.
Nelson alifariki saa 7 na dk 35 p.m mkewe akiwa pembeni yake. Na safari ya Baby Face Nelson ikaishia hapo akiwa na miaka 26 tu.
Mwili wa Nelson uligunduliwa na FBI Walter Walsh ukiwa umefunikwa/ viringishwa blanket mbele ya makaburi ya kanisa la Lutheran, St. Paul in Skokie. Hellen alidai alimfunika blanket Nelson kwa sababu alichukia baridi, " he always hated being cold ".
Mwili wa Nelson ulikutwa na matundu 17 ya risasi, nyingi zikimpata miguuni huku iliyomuua ikiwa ni ile aliyopigwa na Cowley ikampata tumboni, ikapita kwenye ini hadi kwenye kongosho na kutokea mgongoni.
Hollis alifariki mara tu baada ya kufikishwa hospitali, kwenye hospitali nyingine Cowley alifanyiwa upasuaji lakini alifariki kwa jeraha kama lililomuua Nelson... risasi ya tumbo.
Mkuu wa FBI kipindi hicho J. Edgar Hoover aliamuru mke wa Nelson atafutwe, akitoa amri ya mkimuoa tu ueni. "find the woman and give her no quarter ".
Hellen akiwa ndio public enemy wa kwanza mwananke katika historia ya Marekani alijisalimisha mwenyewe siku ya thanksgiving na akahukumiwa mwaka 1 kwa kumlea mumewe akiwa majeruhi huku akijua na jambazi na anatafutwa.
John Paul Chase nae alikamatwa na kupelekwa gereza la watukutu alcatraz.
Hiyo ndio historia ya Baby Face Nelson...
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena