Benki kuu Tanzania imepunguza kiwango cha riba kwa mabenki ya biashara kufikia asilimia 11.
Hatua hiyo inadaiwa itawezesha mabenki ya biashara kupunguza gharama za kukopa fedha benki kuu hivyo kutoa uwezekano wa kupunguza riba kwa wateja wao pia serikali ilichukua hatua ya kupunguza kiasi cha fedha ambacho mabenki ya biashara ilikuwa ikitunza Benki Kuu(Statutory minimum reserve ratio) kutoka asilimia 10 mpaka nane ili kuziwezesha benki kuwa na fedha zaidi kwa ajili ya kukopesha.
Katika hatua nyingine, riba za dhamana za serikali zimepunguzwa kufikia wastani wa asilimia sita, hatua hiyo itapunguza mabenki kufanya biashara na serikali na badala yake kuwakopesha watu wa kawaida kutokana na faida ya kuikopesha serikali kuwa ndogo sana ukilinganisha na kukopesha watu wa kawaida.
Naibu gavana wa Benki kuu, Dr. Kibesse amesema benki kuu imekuwa ikichukua hatua hizo ili kuwawezesha wananchi wamudu kukopa ndio maana kiwango cha riba kimekuwa kikishuka.
Akiwa kwenye kikao na wafanyabiashara Ikulu Juzi, Rais Magufuli alielezea azma ya serikali kufanya fedha yake kuwa ngumu kwa mabenki ili warudi kwa wananchi ikiwemo kupunguza kutoa hati fungani za serikali kwa mabenki
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena