Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MAKALA | Tunakaribia Kuishi Nje ya Sayari ya Dunia - The Bold

Image result for space colonization
Mfano wa makazi ya chini ya ardhi katika sayati ya mars ambayo yanayopendekezwa
Image result for elon musk
Mwanasayansi Elon Musk


TUNAKARIBIA KUISHI NJE YA SAYARI DUNIA

Ni zaidi ya miaka ishirini sasa tangu ‘Mars Pathfinder’, chombo cha kwanza cha utafiti kutua kwa mafanikio kwenye sayari ya mars na kutuma taarifa duniani. Mafanikio yale yametufungua macho juu ya mambo mengi ambayo tulikuwa hatuyajui kuhusu sayari hii nyekundu na pia imeleta hamasa mpya ya kutaka kuishi ndani yake.

Mwishoni mwa mwaka jana,mwezi desemba moja kati ya habari ambazo zilitawala sana vyombo vya habari ilikuwa ni kufanikiwa kwa kurushwa tena kwa mara nyingine kwa rocket ya Falcon 9 ya kampuni ya SpaceX ya bilionea Elon Musk. Hii likuwa ni mara nyingine tena kwa mwaka jana kwa kampuni ya SpaceX kutumia rocket moja zaidi ya mora moja kuirusha kwenda angani. Kwa mfano roketi hii ya Falcon 9 iliwahi kutumiaka mwaka jana mwezi February kupeleka vifaa angani juu katika International Space Station. Safari hii pia, yaani mwezi huu desemba ilitumika kuweka satelaiti ya EchoStar/SES-11 katika anga.
Kwa mwaka jana pekee hii ilikuwa ni mara ya kumi na tano kwa kampuni ya SpaceX kurusha roketi angani. Jambo la msingi zaidi hii ilikuwa ni mara nyingine tena ambapo SpaceX wamefanikiwa kutumia roketi zaidi ya mara moja. Yaani kuweza kurusha roketi angani na kisha roketi hiyo kurejea duniani na kutumika tena katika misheni nyingine kwenda angani.

Uwezekano huu mpya wa roketi kubwa na nzito kutumika zaidi ya mara moja inatatua moja ya changamoto kuu zaidi ambayo ilikuwainaleta mkwamo kwenye tafiti za nje ya sayari… changamoto ya gharama za kuunda roketi mpya kila utakapo kurusha chombo kwenda angani.
Image result for falcon 9
Hii ni mfululizo wa viashiria vya nadhiri ambayo bilionea kijana na mwenye hamasa kubwa, Elon Musk na kampuni yake ambayo wameiweka kuhakikisha kwamba wanafanikiwa kupeleka binadamu wa kwanza kwenye sayari ndani ya muda mfupi ujao na kwa gharama nafuu zaidi. Elon Musk mwenyewe amewahi kukaririwa akisema kwamba kampuni yake imedhamiria kuunda roketi ya injini 42 ambayo itakuwa na uwezo wa kubeba watu 100 kwenda kwenye sayari hiyo nyekundu.

Swali kubwaambalo binafsi nimekuwa najiuliza kwa kipindi kirefu ni kwamba endapo tutafanikiwa kupeleka binadamu kwenye sayari ya Mars, ni namna gani maisha yatawezekana huko? Je, baada ya mika kadhaa (labda elfu kadhaa) baada ya kuwa tumeishi Mars, je sayari hii tutaweza kusababisha hali ya sayari hiyo kubadilika ili kuendana na uwepo wa wakazi wapya au labda ni sisi ambao tumeenda kwenye sayari hiyo tutapaswa kubadilika walau namna yetu ya kuishi ili kuendana na mazingira ya sayari hiyo?

Suala la kupeleka binadamu sayari ya Mars na hatimaye kuweza kuishi kwenye sayari hiyo sio hadithi tena au visa tu kwenye filamu za kimagharibi bali kwa sasa limekuwa ni suala halisi kabisa huku mabilioni ya dola za kimarekani zikiwekezwa na serikali na watu binafsi ili kuweza kufanikisha suala hilo. Kituo cha anga cha serikali ya marekani wanakadiria kwamba mpaka kufikia mwaka 2030 watakuwa wamefanikiwa kupeleka binadamu kwenye sayari ya Mars, lakini bilionea Elon Musk na kampuni yake ya SpaceX wao wametoa uhakika kwamba mpaka kufiia mwaka 2023 tu wao watakuwa wamefanikiwa kupeleka mtu kwenye sayari hiyo. Kwa hiyo suala la kupeleka binadamu sayari ya Mars halina ubishi tena… litatokea, tena laweza kutokea mapema kuzidi tunavyofikiri.

Lakini je, wanasayansi hawa wamejiandaa vipi kukabiliana na hali ya sayari ya Mars? Sayari ambayo juu ya ardhi yake ni kama hakuna hewa ya oksijeni kabisa, sehemu kubwa ikiwa ni hewa ya carbon dioxide? Saayari ambayo nguvu yake ya mvutano ni sawa na 38% tu ya nguvu ya mvutano ya dunia? Sayari ambayo ‘atmosphere’ yake ni sawa na 1% tu ya atmosphere ya dunia kutoka usawa wa bahari? Sayari ambayo ina baridi kali kupitiliza kiasi kwamba kiumbe hakiwezi kuishi na mabadiliko makubwa ya haraka ya joto ndani ya muda mfupi. Kwa mafano muda wa mchana joto laweza kupanda mpaka nyuzi joto 20 za Celsius na ndani ya muda mfupi joto likashuka mpaka nyuzi joto hasi 100 za celsius… na si hivyo tu bali pia kutokana na wembamba wa atmosphere yake mionzi ya jua inapenya zaidi kwenye sayari hii kuzidi hapa duniani.
Hata wanasayansi walipogundua kwamba kuna uwezekano wa mamilioni ya miaka kwamba sayari hiyo ilikuwa na maji, na kama kuna H2O basi sehemu hiyo yawezekana kuishi. Lakini papo hapo wanasayansi hao waking’amua kwamba hata kama sayari hiyo ingalikuwa na maji mamilioni ya miaka iliyopita, lakini kutokana na muundo wa hewa yake juu ya ardhi na asili yake ya udongo ni lazima maji hayo yalikuwa na chumvi kupitiliza au tindikali nyingi kiasi kwamba isingeliwezekana kuwezesha uhai kuwepo.

Lakini badi viko vidhibiti vingine kama vile dalili ya mabaki ya minyoo kwenye miamba ambayo inashiria kwamba yawezekana palipata kuwepo uhai kwenye sayari hii, lakini pia upande mwingine kuna viashiria vingine vya kisayansi pia ambavyo vinatuonyesha kwamba kuna uwezekano hakujapata kuwepo uhai kwenye sayari hii.

Lakini tumekwisha dhamiria kwamba lazima twende mars. Na si kwenda tu, bali lazima tufanikiwe kuishi ndani yake? Vipi ‘mabwana wakubwa’ hawa wanafanya nini kutufanikisha kwenye hilo? Maandalizi yakoje?

Kwanza kabisa nianishe kwamba ili tuweze kuishi katika sayari ya Mars kuna vitu kadhaa muhimu ambavyo ni vya lazima, yaani kwamba tutahitaji;
- Hewa
- Chakula
- Maji
- Makazi
- Choo
- Malazi
- Joto sahihi
- Kuweka mwili safi (mfano kuoga)

Sasa ni namna gani ambavyo tutaweza kukabiliana na haya?

Kwa miaka mingi sana sasa, kituo cha masuala ya anga cha serikali ya Marekani, NASA wamekuwa wakifanya tafiti na majaribio ya kuunda bunifu ambazo tunaweza kuzitumia kutuwezesha kuishi katika sayari ya Mars. Kutokana na utofauti wa hali ya Mars kama ambavyo nimeeleza hapo juu, mapendekezo makuu ya bunifu hizi ni kuwezesha kuweka makazi Mars ambayo eidha yatakuwa chini ya ardhi au kuunda makazi juu ya ardhi ambayo yako ‘sealed’ yakijitosheleza ndani kwa kila kitu.

Mfano wa makazi ya chini ya ardhi katika sayati ya mars ambayo yanayopendekezwa
Image result for martian habitatKwa mfano ili kuweza kutengeneza mfumo wa uwepo wa chakula tukiwa kwenye makazi hayo ambayo yako sealed na namna ya kuweza kuratibu mfumo wa hewa ya Oksijeni na kaboni dayoksaidi, makazi haya yanaweza kuwa na sehemu ya kutunza mimea ambayo inapaswa kukua kwenye mazingira kama ya kufanana na ‘green house’. Lakini kwa kuzingatia nguvu ndogo ya mkandamizo (pressure), viwango tofauti vya joto, utofauti mkubwa wa pH na mwanga wa jua, ni lazima kuwa na mmea ambao utaweza kuhimili tofauti hizi na uwe na uwezo wa kukua kwa haraka na kutoa kiwango kidogo sana cha uchafu. Ndipo hapa ambao wanasayansi wa NASA wanafikiria kuweka kwenye makazi haya mimea rahisi kama vile ‘duckweed’ au ‘Azolla filiculoides’ (water fern). Hii ni moja kati aya mimea rahisi zaidi katika muundo wake wa kibailojia… nadhani wengi tunaweza kuwa tumewahi kuiona labda majina tu haya ndiyo yanaweza kuleta mushkeli. Huwa inakua juu ya mabwawa au madimbwi makubwa ya maji yaliyotuama kwa muda mrefu.

Lakini suala lingine ambalo wanasayansi hawa wanafikiria katika kuunda makazi haya ni namna ambavyo tabaka la hewa (atmosphere) litatakavyoundwa ndani ya makazi hayo pamoja na ujoto wa tabaka hilo la hewa. Moja ya mapendekezo yaliyoko ni kwamba makazi hayo yaweze kuwa na mfumo wa kuweza kuchukua hewa ya nitrogen na argon kutoka kwenye anga la Mars. Lakini pendekezo hili changamoto yake kuu ni ugumu wa kuzitenganisha hewa hizi. Ndipo hapa ambapo wanasayansi hawa wanadhani kwamba ni vyema zaidi tabaka la hewa likawa na mchanganyiko wa 40% ya hewa ya argon, 40% hewa ya nitrogen na 20% hewa ya oxygen. Hii itasaidia kupata mchanganyiko wa ‘Argox’ ambao inawezekana kabisa kutumika kwa ajili ya upumuaji. Argox ingali inatumika hata sasa katika teknolojia za mitungi ya wapiga mbizi baharini. 

Lakini si hivyo tu, kutokana na utofauti huu wa sayari ya Mars wanasayansi pia wameanza kufikiria uwezekano wa namna ya kuweza kuibadili ardhi ya juu ya sayari ya mars (regolith) ili iweze kuendana na hii ya duniani. Kama suala hili litafanikiwa basi itasaidia kwa mfano kuweza kukuza mazao juu ya ardhi ya mars yenyewe (badala ya ndani ya makazi) na kama tutaweza kukuza mimea juu ya ardhi ya mars basi tutafanikiwa kwa kiwango kikubwa kubadili muundo wa hewa iliyoko mars na hata hali ya hewa yake.

Ili kufanikisha kubadili ardhi ya juu ya mars, wanasayansi hawa wanafikiria kupeleka bacteria aina ya ‘cynobacteria chroococcidiopsis’ ambao wataachiwa kwa wingi juu ya ardhi ya mars. Bacteria hawa wana sifa ya kuweza kuishi kwenye mazingira yenye joto kali au baridi kali kupitiliza. Lengo kuu hapa ni kwamba, bacteria hawa wataendelea kuzaliana na wengine kufa na kuongezeka zaidi na kuendelea kufa zaidi na kuzaliana zaidi. Wale bacteria ambao wanakufa wanasaidia kutengeneza ‘organic layer’ kwenye udongo wa juu wa sayari ya mars. Kwa hiyo miaka kadhaa baadae tabaka la juu ya udongo wa mars unaweza kuwa na hali fulani nzuri ya kufanana na udongo wa dunia japo kwa uchache tu.
Hivi karibuni pia kuna aina ya fungi aitwaye ‘cryptoendolithic fungi’ ameweza kuishi kwa muda wa miezi 18 katika mazingira yaliyotengenezwa kufanana kabisa na mars. Kwa hiyo wanasayansi wanaweza pia kutumia fungi huyu kumpeleka kwenye ardhi ya mars ili baada ya miaka kadhaa tuwe na organic layer juu ya udongo wa sayari hiyo.

Suala la mwisho la msingi sana ambalo wanasayansi wanakuna mbongo kuona namna gani linafanyika, ni kujaribu kutazama namna ambavyo tutaweza kutumia rasilimali za mars ili tuweze kujikimu pasipo kutegemea kusafirisha vitu kutoka duniani kwenda mars.
Kwa mfano kuna baadhi ya mabonde ya mars yanasemekana kwamba yana maji. Tunaweza kutumi maji haya kwa kuyatenganisha na kupata hewa ya hydrogen na oxygen. Oxygen yaweza kuchanganywa na nitrogen na argon kuunda hewa ambayo tutatumia kupuma huku hydrogen inaweza kuchanganywa na carbon dioxide kuunda plastic au methane. Plastic tunaweza kutumia kuzalisha vitu ambavyo twahitaji kwenye makazi na methane yaweza kubadilishwa zaidi kwa kutumia Sabatier process na kutumiaka kama chanzo cha nishati. Kama tutaweza kufanya hivi (kutumia methane kama chanzo cha nishati) hii itatusaidia kuondoa utegemezi juu ya kusafirisha solar panel mpaka mars ambazo zitakumbwana changamoto ya kufunikwa na vumbi kwa sababu itatulazimu kuziweka nje ya makazi. Sayari ya mars ina vumbi kali muda wote. Ubaya wake ni kwamba vumbi lake ni jembamba mno (kama vile wembamba wa moshi wa sigara kwa mfano) hivyo ni ngumu sana ulidhibiti nah ii itapunguza ufanisi wa solar panels.
Image result for martian habitat
Hii ni 'Biodome' ambayo inapendekezwa kwamba inaweza kutumika katika sayaro ya mars


Mobile Habitat; haya ni moja ya makazi yanayopendekezwa kutumiwa na watafiti wa kwanza watakaofika mars kwa ajili ya kuwawezesha kuizunguka sayari hiyo na kuitafiti kwa undani zaidi
Related image


Niseme tu kwamba, kama ilivyo dhahiri changamoto ni nyingi sana mpaka siku ambayo tutafikia hatua ya binadamu kuishi katika sayari ya mars na hata changamoto nyingine sijazigusia kabisa katika andishi hili fupi. Lakini ni ukweli ulio dhahiri kabisa kwamba binadamu tumejaliwa akili kubwa na uwezo wa kuwa ving’ang’anizi mpaka kufanikisha jambo. Yawezekana isiwe leo, au isiwe kesho au mwakani au miaka kumi ijayo. Labda ni watoto wetu, au labda wajukuu zetu au wajukuu wa watoto wetu… lakini binafsi nina imani pasina shaka kabisa, juhudi hizi tunazoziweka sasa zitazaa matunda… na iko siku binadamu ataishi nje ya sayari dunia


Hii ni ESO Hotel. Ni kituo cha utafiti kilichopo kwenye jangwa la chile ambapo sehemu yenye majengo haya kwa hali ya hewa ina mfanano kiasi na Mars. Picha ya mwisho chini ni 'Biodome' ambayo iko kwenye kituo hicho. Tafiti na gunduzi ambazo zinafanyika kwenye kituo hiki na hii biodome inaweza kusaidia sana kutumia katika kuunda makazi ya Mars
Image result for ESO Hotel

Imeandikwa na Habib Anga (The Bold) | RoryaFinest.Com

Post a Comment

0 Comments