Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Kwenye Hekaheka ya leo:inatoka Morogoro. Nesi aliruhusu mtoto aliyezaliwa kuzikwa kumbe alikuwa hai

light_for_charlie1
Hekaheka ya leo January 06 inatoka Morogoro, mama mmoja mjamzito alikwenda Hospitali ya Mkoa Morogoro siku ya jana, alipofika hospitali hapo hakupata huduma nzuri kutoka kwa nesi aliyekuwa zamu, baada ya uchungu kumshika alihangaika bila msaada wowote na mwisho wake akajifungua chini.
Wakati huo ilikuwa usiku, umeme ulikuwa umekatika na wakalazimika kutumia tochi ya kwenye simu wakati akijifungua.
Nesi huyo alikuja kumpa msaada baadaye akamwambia kwamba tayari mtoto wake ameshafariki, hivyo awaite ndugu zake ili wamchukue mtoto huyo wakazike.
Ndugu walimchukua mtoto huyo akiwa amewekwa ndani ya  ndoo, walipofika nyumbani waligundua kwamba mtoto alikuwa mzima bado lakini waliporudi tena Hospitali jitihada za kumtibu hazikusaidia kwani alifariki wakati wakianza jitihada za kumshughulikia.
Mganga Mkuu Hospitali ya Mkoa Morogoro amesema kuwa hakuwepo kwa kuwa yupo likizo.
Isikilize hapa Hekaheka yote kwa kubonyeza play.

Post a Comment

0 Comments