Simu za Nokia ni moja
ya simu ambazo zimekuwa na umaarufu mkubwa Duniani, mbali na hiyo hii ni
moja ya Kampuni kongwe zaidi kwenye soko la bidhaa hizo.
Kuna wakati ambao umaarufu wa bidhaa za Nokia ulishuka, lakini unaambiwa kwa sasa wanakuja hivi; Nokia wametengeneza simu za Nokia 215, zitakuwa za line moja na line mbili.
Simu aina hii ina uwezo mkubwa wa kukaa
na chaji mpaka mwezi mmoja kwa ile ya line moja, ya line mbili ina uwezo
wa kukaa na chaji kwa siku 21, zina internet na mtumiaji ataweza
kutumia Facebook, Twitter ambazo zimeungwa moja kwa moja tofauti na ilivyo kwa smartphone.
Wanakadilia kwamba zikiingia sokoni bei yake itakuwa ni dola 29, ambayo ni sawa na sh. elfu 50 kwa T’zania.
Microsoft wamepanga kuiuza simu hii Afrika, Asia, Ulaya, na Mashariki ya Kati japo hawajasema lini itakuwa sokoni.
Hii ni moja ya hatua kubwa ambazo Nokia imezipiga sokoni tangu Kampuni hiyo inunuliwe na Microsoft.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena