Header Ads Widget

Responsive Advertisement

MIVARF NA OWECO WAPANIIA KUWAINUA WAKULIMA WA MPUNGA RORYA


Mratibu wa Mradi huo Bwana Benjamin Amosi akitoa ufafanuzi juu ya mikakati ya mradi huo
Shirika la IWECO kwa kushirikiana na MIVARF wameendesha warsha kwa vikundi vya wakulima wa mpunga kwa kata za Komuge, Rabuor na Nyathorogo kwa Vijiji vya Chereche, Irienyi Ochuna na Komuge ambavyo vimo katika mradi wa Skimu
Akielezea umuhimu wa kamati hizo, Mratibu wa mradi huo ndugu Benjamin Amosi amesema Kamati za masoko zina kazi ya kuhakikisha kwamba wakulima/wanavikundi wanapata soko la uhakika ili kuondokana na tatizo la wakulima kudhulumiwa haki zao wakati wa mavuno.


Afisa Kilimo Bwana Emmanel Rutatora akitoa elimu kwa vikundi
Naye afisa ushirika wa wilaya ya Rorya Bwana Emmanuel Rutatora  amewaeleza wanakamati kwamba umuhimu wa kuanzisha chombo cha fedha kama SACCOS ama vikundi vya hisa ili kujiwekea utaratibu wa kukopeshana wakati wa kilimo ili kuondokana na wafanyabiashara ambao huwadhulumu kwa kuwakopesha wakulima kwa riba ndogo ya 50% kitu ambacho mkulima hakiwezi kumsaidia mkulima kujikwamua kiuchumi.
Ndugu Elias Eliud wa Irienyi aliongeza kwamba mradi utawajengea lini stoo ya kutunzia mpunga, akijibu swali hilo Afisa ushirika ndugu Rutatora alieleza ya kwamba ili kujenga stoo, wakulima wanatakiwa kujiwekea utaratibu wa kutenga sehemmu ya faida ya mapato yao na baadaye serikali na wahisani wataongeza na kuwaongezea nguvu katika  juhudi zao.

Wananchi wakifuatilia warsha hiyo

Post a Comment

0 Comments