Waziri mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi ya vyakula vya Kitanzania vilivyosindikwa kitalaamu, Afisa Mtendaji Mkuu na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Sumitomo ya Japan,Bw.Michihiko Kanegae baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya New Otani, Tokyo, Machi 16, 2015. Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza ujenzi wa mtambo wa kufua umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyerezi jijini Dar es salaam hivi karibuni. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Masuala ya Miundombinu ya Umeme wa kampuni hiyo, Tsutomu Ben Akimoto. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na ujumbe wake wakiagana na Afisa Mtendaji Mkuu na mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Sumitomo Corporation Corporation ya Japan,Bw.Michihiko Kanegae (wapili kushoto) baada ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya New Otani, Tokyo, Machi 16, 2015. Kampuni hiyo inatarajiwa kuanza ujenzi wa mtambo wa kufua umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyrezi jijini Dar es salaam hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Japan aliyemaliza kuda wake, Salome Sijaona, Waziri wa Nchi, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Abood Mohamed na Balozi mpya wa Tanzania nchini Japan, Batilda Burian.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata Maelezo kutoka kwa Ofisa wa Ubalozi wa Japan nchini Tanzania, Noriko Tanaka kuhusu Treni inayofanyakazi bila dereva katika jiji la Tokyo wakati alipotembelea Ofisi za Kampuni inayoendesha treni za aina hiyo ili kujifunza namna ya kusafirisha abiria kwa njia ya reli katika majiji Machi 16, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipata maelezo kutoka kwa Mbunge na Naibu Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Bw.Shigeki Iwai kuhusu kipeperushi chenye picha zinazoonyesha kilimo cha chai kuzunguka mlima Fuji nchini Japan katika mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye hoteli ya New Otani, Tokyo Machi 16, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena