Akubaini kuwa ndoto yake ya maisha ilikuwa inatimia kwa mwendo wa kinyonga. Akaamua kununua mashine ya kutengeneza mishumaa. Tangu hapo hajajuta kwa uamuzi huo.
“Kuna mambo mengi mtu angetamani kuyafanya maishani lakini kwa mshahara mtu anaishindwa kufikia malengo yake kwa muda alioupanga. Ndio maana nikachukua akiba yangu nikawekeza katika mashine ya kutengeneza mishumaa” alisema Muhwezi.
“Hii kazi nilianza miaka 3 iliyopita baada ya kuhudhuruia kozi ya miezi 6 huko Nairobi, nikapata cheti cha utengenezaji mishumaa, sabuni na bidhaa nyinginezo zinazofanana”. Alisema Muhwezi.
Na wakati aliporejea toka Nairobi ndipo alipo nunua mashine hiyo kwa Sh. 8,000,000/= na akaanza kutengeneza mishumaa kwa jina la Safe Candles yaani, Mishumaa Salama.
Mishumaa hutengeenzwaje?
“Tunatumia wax (nta) tunayoinunua kwenye maboksi ya Kg 25. Na kila mzunguko mmoja wa uzalishaji hutumia Kg 5, hivyo kwa boksi moja huenda mizunguko mitano. Tunatengeneza mishumaa 120 kwa mzunguko mmoja “ alielezea Mhwezi.
Mashine ya kutengeneza mishumaa huendeshwa kwa mkono na malighafi yake ni nta ya mishumaa (candle wax).
Utambi ndio huwasha mshumaa. Wax hununuliwa kwenye maduka ya kilimo mjini ambapo hupimwa katika kilo. Mchakato unaanza kwa kuyeyusha wax kwa moto. Mashine ina usukani ambao hutumika kuigeuza mashine ili matundu yake yafunguke kwa ukamilifu na kujitokeza kwa nje.
Hivyo nta (wax) ikiishayeyuka hutiwa ndani ya matundu. Mashine imeunganishwa na tanki la maji ambalo hufunguliwa wakati nta ikiwa tayari imejazwa kwenye matundu ili kuipoza na kuigandisha na kuwa mishumaa.
Baada ya dakika 30 – 40 bomba la kutoa maji kwenye mashine hufunguliwa ili kuyarejesha maji kwenye tanki . Gurudumu huzungushwa kushoto ili kuitoa mishumaa nje ya mashine.
Manufaa.
Mashine hii huendeshwa kwa mkono haitumii umeme wala mafuta na pia ni ndogo kwa umbo hivyo huchukua eneo dogo sana la chumba.
Ukuaji wa biashara.
Muhwezi amesema, “ Tulianza biashara kwa kuuza mlango hadi mlango kwa wateja wadogo, lakini sasa, wateja wanatumia mawasiliano, hupiga simu na kuweka oda za kutengenezewa. Kwa sasa, Muhwezi amefungua maduka Entebbe, Masaka na Burundi ambako wateja wake hufuata bidhaa ya mshumaa. Aidha, amefanikiwa kusajili kampuni ya utengenezaji mishumaa kwa jina la Lwenu Group of Companies.
Muhwezi amefanikiwa kiuchumu toka kwenye kipato cha Sh. 500,000 kwa mwezi alipoajiriwa na Hoteli hadi kupata Sh. 2.5 milioni kwa wiki hii imemuwezesha kuweza kutunza familia yake, pia amefungua biashara ya utengenezaji sabuni na biashara ya ukopeshaji fedha.
Kitu gani huifanya mishumaa yake iwe ya kipekee?
“Mishumaa yetu haiyeyuki na pia inafukuza mbu. Hii imeifanya mishumaa yetu kupendwa na kushinda ushindani wa soko”.
“Mishumaa yetu hudumu kwa kuwa haiyeyuki” aliongeza Muhwezi.
Fursa.
Muhwezi ameamua kushirikisha wengine kunufaika na mafanikio yake. Miaka miwili iliyopita, alianza kufundisha Wanafunzi Mashuleni na pia Wafanyakazi kutoka Asasi mbali mbali, hususani Asasi za Wanawake. Alifundisha jinsi ya kutengeneza mishumaa, hadi sasa imemlipa vizuri.
Changamoto.
“Kodi kubwa kwenye wax imefanya wax iwe ghali na hivyo kuzidisha gharama za uzalishaji. Ukosefu wa maji nao ni changamoto. Wakati mwingine, hatuna maji eneo hili, mashine inahitaji maji yenye mkandamizo mkubwa”.
Pia, anashindana na wawekezaji wa kigeni ambao wana misamaha ya kodi na vivutio vingine toka serikalini. Hii imewafanya wawekezaji kunufaika kwa kuzalisha mishumaa kwa gharama ndogo na kupata faida kubwa ukilinganisha na kina Muhwezi.
Mipango.
Nataka kufungua shule ya kufundisha kutengeneza mishumaa, sabuni na sabuni ya unga, nimepanga pia kununua mashine ya kutengeneza chocolate.
www.njiampya.com
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena