Header Ads Widget

Responsive Advertisement

AFYA YAKO LEO | FAHAMU TIBA ASILIA YA UGONJWA WA PRESHA.

Shinikizo la damu (presha) kitaalam huitwa Hypertension au High Blood Pressure kwa jina la kawaida shinikizo la damu. 


Shinikizo la damu kwa kawaida hutokea endapo msukumo wa damu katika kuta za mishipa ya damu unapoongezeka kutokana na mishipa ya kusafirisha damu kuziba au kuwa midogo na kushindwa kupitisha damu kama inavyotakiwa. 


Hali hiyo husababisha moyo kufanye kazi zaidi kuliko kawaida ili kuzungusha damu mwilini. 

Kimsingi shinikizo la damu ni tofauti na shinikizo la kawaida la damu linalotakiwa katika mwili wa binadamu ambalo linaongeza msukumo wa damu katika kuta za damu mwilini. 

Mara nyingi ugonjwa huu huwa hauna dalili za moja kwa moja, lakini baadhi ya watu wenye shinikizo la damu la juu hupata maumivu ya kichwa hasa upande wa nyuma ya kichwa hasa asubuhi, wengine huisi kizunguzungu nk. 

Hata hivyo zipo njia za kuepuka ugonjwa huu ambazo ni pamoja na watu kubadilisha mfumo wa maisha. Ikiwa ni pamoja na kuzingatia ulaji bora wa chakula hasa vyakula vya asili pamoja na kufanya mazoezi,. 

Mgonjwa wa shinikizo la damu la juu hupaswa kuepuka kula chumvi na mengine ambayo atashauriwa na daktari. 

Kitunguu swaumu ni moja ya kiungo ambacho huweza kutoa ahueni kwa mtu mwenye tatizo la presha. Unachopaswa kufanya ni kupata punje 5 za kitunguu swaumu na uchanganye na maji lita moja kisha chemsha maji hayo yakiwa pamoja na kitunguu swaumu. 

Baada ya kuchemka vizuri yaache maji hayo yapoe, kisha mhusika yaani yule mtu mwenye tatizo la presha atumie mchanganyiko huo ndani ya wiki 3 hadi 4 mfululizo.

Post a Comment

0 Comments