Jeshi nchini Nigeria linasema kuwa
kumetokea mlipuko mkubwa katika soko moja kaskazini mashariki mwa jimbo
la Borno ambapo watu 47 wamefariki huku wengine 55 wakijeruhiwa katika
mji wa sabon gari.
Haijulikani iwapo mlipuko huo ulisababishwa na mlipuaji wa kujitolea muhanga ama kilipuzi kilichotegwa katika soko hilo.Kundi la Boko Haram limekuwa likitekeleza mashambulio katika eneo lote la kaskazini mashariki mwa Nigeria
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena