Nimekutana na stori moja kutoka Nigeria ambako Polisi aliyekuwa kazini amekamatwa baada ya picha inayomuonyesha akiwa amelewa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Taarifa hiyo ilisambaa na kumfikia Lagos State Police Commissioner CP Fatai Owoseni
baada ya watu wengi kupitia mitandao ya kijamii kuhoji mara mbili mbili
uadilifu wa mapolisi hao huku wakidai kitendo hicho kinaleta picha
mbaya kwa jamii wanayoizuguka.
Kwa sasa polisi huyo yupo chini ya ulinzi na Police Commissioner ameagiza uchunguzi wa kina dhidi yake ufanyike huku polisi huyo akiwa matatani kufukuzwa kazi ama kupewa adhabu kali.
Polisi Commissioner wa Lagos amesema
polisi huyu atakuwa mfano kwa mapolisi wengine amabao hawachukuli kazi
zao serious licha ya kuwasihi kutokujihusisha na vitendo vinavyoenda
kinyume na sheria zao za kazi ikiwemo sheria iayomzuia polisi kutumia
kilevi cha aina yoyote akiwa kazini.
Commissioner wa Polisi Lagos amewashukuru
raia wenye matumizi ya mitandao ya kijamii huku akiwasisitiza kuendelea
kutoa support zao kwa kuendelea kuwaweka hadharani mapolisi wengine
wanaoenda kinyume na wajibu wao wa kiserikali.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena