Bila shaka matokeo ya utafiti huu yatawashangaza watu wa nchi nyingine,
lakini sio sie Watanzania, ambao tumebainika kuwa watu wanafiki zaidi
kuliko wote duniani. Sio jambo la kushangaza kwa sababu unafiki umekuwa
sehemu ya utamaduni wetu.
Na mfano mwepesi wa unafiki wetu ni kuhusu uamuzi wa serikali kuipiga
marufuku video ya msanii Snura iitwayo 'Chura' ambayo ilivuka mipaka ya
ustaarabu. Awali, watu wengi waliishutumu Serikali kwa kuruhusu video
hiyo 'chafu' kuonyeshwa ilhali vikao vya bunge vikizuiwa kuonyeshwa
'live.' Well, japo bunge laendelea 'kufichwa,' lakini serikali
imejitutumua na kipiga kufuli video ya 'Chura.'
Lakini hatua hiyo imewakera baadhi ya wenzetu. Wengine wanadai serikali
ina vitu muhimu zaidi vya kufanya badala ya kufungia video. Wengine
wanadai mbona kuna video chafu zaidi za 'akina Rihanna' kuliko hiyo ya
Chura. Wengine wanakwenda mbali na kudai kuwa alichofanya Snura na hao
mabinti wa kwenye video ni UBUNIFU. Really?????
Twende kwenye maisha yetu ya kila siku. Tuchukulie mfano vifo. Utakuta
watu wanasubiri mpaka mtu afe ndio waanze kumwagia sifa, "Oh marehemu
alikuwa mtu mzuri sana, oh marehemu alikuwa mwema sana...RIP...RIP..."
Hii tabia ya kuwapenda watu wakifa lakini kuwachukia walipokuwa hai ni
nini kama sio UNAFIKI? Angalia Marehemu Kanumba alivyoandamwa wakati wa
uhai wake. Msanii aliyefanya kazi kubwa kabisa kuiinua medani ya filamu
za Kitanzania aliandamwa mfululizo na hili na lile, huku watu wasio na
vipaji ya kitu chochote kile wakigeuka mahakimu na majaji dhidi ya
kipaji cha msanii huyo.
Tuangalie huko mitaani tunakoishi na 'makazi yetu mapya' mitandaoni.
Huko mitaani, wenzetu wenye umuhimu mkubwa kwa jamii - madaktari,
manesi, walimu, nk - hawapewi heshima kubwa kulinganisha na wanayopewa
wahalifu kama wauza madawa ya kulevya au wabadhirifu serikalini. Twaita
wauza unga WAZUNGU WA UNGA, na wabadhirifu twawaita MAPEDEJEE, VIBOSILE,
VIGOGO, na majina mengine ya kuwatukuza, ilhali jina lao stahili ni
WAHALIFU.
Nenda mtandaoni, kwa mfano Instagram. Ukiacha wasanii wetu na watu
wengine muhimu, watu maarufu zaidi katika mtandao huo kwa Tanzania ni
wale wenye kuongoza makundi ya matusi, picha za utupu, majungu, na
madudu kama hayo. Sio kwamba hawa 'wameroga' ili kuwa maarufu. Hapana.
Umaarufu wao unatokana na Watanzani wengin kupenda vitu hivyo: picha za
utupu, majungu, nk.
Angalia wakati wa uchaguzi. Wanasiasa wetu hujiweka karibu kabisa na
wananchi. Si ajabu kuona mwanasiasa akiwasalimia wananchi kwa kupiga
magoti 'kwa heshima' wakati anaomba kura.Subiri ashinde uchaguzi.
Humsikii japo akicheka au kuzomea bungeni. Unaweza kuhisi kuwa asilimia
kuwab ya wabunge wetu wanatoka majimbo ya nchi kama Uingereza au
Marekani, ambazo zina matatizo machache kwa wapigakura, kwani haiingii
akilini kwa mbunge ambaye jimbo lake lina matatizo lukuki awe haonekani
bungeni unless kwenye kukusanya posho tu, na akitokea bungeni, si ajabu
kuona amepigwa picha huku kachapa usingizi (labda alishindwa kulala
kutokana na kuzongwa na mawazo kuhusu jimbo lake?)
Anyway, turudi kwenye utafiti unathibitisha tulivyobobea kwa unafiki.
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Nottingham cha hapa Uingereza waliendesha
utafiti wa kupima kushamiri kwa ukiukwaji wa kanuni katika nchi 159
duniani, wakitumia takwimu za kutoka mwaka 2003 kuhusu ubadhirifu katika
siasa, ukwepaji kodi na rushwa.
Twende tena mtaani. Kuna suala la ushoga ambalo taarifa zinaeleza kuwa
unakua kwa kasi huko nyumbani. Juzi kuna shoga mmoja kafiwa Dar, na
inaelezwa kuwa takriban kila mtu maarufu jijini hapo hakukosekana
msibani. Lakini sio katika msiba huo tu, nenda Instagram halafu angalia
akaunti za mashoga na idadi ya 'followers' wao. Hivi yawezekanaje kama
'ushoga sio tu ni laana bali pia ni kinyume cha sheria za Tanzania,'
then shoga awe na 'followers' zaidi ya laki moja? Kwanini kila shughuli
ya mastaa wetu haiwi kamili bila uwepo wa mashoga wa 'kukata viuno'
kwenye shughuli hiyo?
Habari kamili kuhusu utafiti huo ipo HAPA na kuna MAKALA HII katika gazeti la kila wiki la RAIA MWEMA Toleo la wiki hii imeandika kwa kirefu kuhusu suala hilo
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena