Meneja wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique yupo mbioni kuchukua mikoba ya Antonio Conte baada ya kikao cha bodi ya klabu ya Chelsea kinachotarajiwa kufanyika leo siku ya Jumanne.
Hatima ya Conte kuondoka Chelsea imetokana na matokeo yasiyo ridhisha dhidi ya Watford siku ya Jumatatu na yale ya Bournemouth.
Habari kutoka Diario Sport zimesema kuwa kocha huyo wa Barcelona, Enrique ni chaguo la kwanza kwa klabu hiyo yenye maskani yake nchini Uingereza.
Enrique mwenye umri wa miaka 47, aliwahi kuzifundisha timu za Roma na Celta Vigo baada ya kutoka Barcelona.
Chombo hicho kimeeleza kuwa timu hiyo imempendekeza beki wazamani wa Barcelona na Chelsea, Juliano Belletti kuwa mkurugenzi wa michezo Stamford Bridge.
Enrique ameisaidia Barcelona kutwaa mataji mawili ya Hispania, matatu ya Spanish Cup na klabu bingwa barani Ulaya mwaka 2015
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena