Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Ujasusi | Umbrella Gun: Usalama wa taifa la Urusi (KGB) walivyoua msaliti wa Bulgaria kwa sumu ya mwamvuli

Image result for poison umbrella
IMG_20180201_123739.jpg 

2059412e708179c9b1adf1bc2a14c869.jpg 

 

Sasa ni miaka mingi sana imepita tangu kuuawa kwa mwanaharakati wa Bulgaria bwana Georgia Markov ambaye aliuawa kwa sumu jijini London mnamo mwezi wa September tarehe 7 mwaka wa 1978.

Mauaji ya bwana Markov ni operation iliyofanywa na idara ya usalama wa taifa ya nchi ya Bulgaria baada ya kupata amri kutoka kwa wazee wa kazi, majasusi wa KGB.

Mauaji dhidi ya Markov yalipelekea kusambaa kwa hasira na malalamiko ulimwenguni kote kwa wakati huo kwa maana aliuawa katikati ya jiji la London, mchana kweupeeee, wakati wa ambao watu wengi husubiria kupanda treni ama mabasi ya umma kwenda kazini.

Aliuwawa na jasusi aliyekuwa na itikadi za kikomunisti ambaye alionekana ana mafunzo maalum ya kuweza kuua kisha kutoroka pasipo kukamatwa wala kujulikana utambulisho wake halisi.

Aliwa ni mzaliwa katika jiji la Sofia, mji mkuu wa Bulgaria, Georgi Markov alisomea industrial chemistry chuo kikuu katika miaka ya 1940 kabla ya kufanya kazi kama chemical engineer na mwalimu katika shule ya ufundi (Technical school) (kama vile Tanga Tech ama Arusha Tech)

Hata hivyo Markov alikuwa ni mpenzi sana wa kazi za fasihi hivyo baadaye akaja kuwa muandishi mashuhuru na wa kuaminika sana wa novels, maigizo pamoja na maigizo yale ya kwenye TV. Kazi zake nyingi za fasihi zilikuwa ni zile za kuikosoa serikali ya ki communist ya Bulgaria.

Markov aliwahi kuandika novel moja aliyoiita kama 'The great roof' pamoja na jina la 'a symbol of the roof of lies' akimaanisha ya kwamba utawala wa serikali ya Bulgaria umejengeka katika misingi ya uongo na kukandamiza mwananchi wake. Matokeo yake ni kwamba hizo novels zikapigwa marufuku na serikali zisichapishwe.

Mnamo mwaka 1969 bwana Markov akaondoka kutoka nchini Bulgaria akahamia nchi za magharibi. Kwanza alianzia Italy kisha akaweka makazi yake ya kudumu jijini London kwenye miaka ya 1970 ambapo akajifunza kiingereza na kisha kufanya kazi kama mwanahabari kwenye idhaa ya ki bulgaria ya shirika la utangazaji la uingereza (BBC) Deutsche Welle (DW) pamoja na Radio Free Europe (Sio Radio Free Africa ya Mwanza hehehehee joking.....)

Baada ya kuwasili United kingdom, Novels nyingi sana za bwana Markov zikawa zinachapishwa na kuigizwa sana katika majukwaa ya sanaa pamoja na TV.

Kitendo cha Markov kukimbilia kwenda ulaya ya magharibi kilimaanisha mara moja ya kwamba huyu bwana alitangazwa ya kuwa ni persona non grata (ikimaanisha haitajiki tena ndani ya Bulgaria) na kufika mwaka 1972 uanachama wake katika umoja wa waandishi wa Bulgaria ulisitishwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 6 jela yeye akiwa hayupo mahakamani (in absentia) kwa kitendo chake cha kuitoroka nchi.

Vitabu vya Markov mbavyo hapo awali vilikuwa vimechapisha, vitaondolewa kutoka maktaba vyote pamoja na maduka ya vitabu na jina lake likapigwa marufuku kutajwa ama kutangazwa katika vyombo vya habari vya Bulgaria.

Hata baada ya kuwa anakaa nje ya nchi, bwana Markov aliendelea kuwa mwiba mkali sana kwa serikali ya Bulgaria kwa kuendelea kuiponda na kuikosoa katika matangazo ya redio kupitia idhaa ya ki Bulgaria ya BBC.

Kuendelea kwake kuikosoa serikali pamoja na chama cha ki communist pamoja na kiongozi wake kulimfanya bwana Markov kuwa adui wa taifa (enemy of the state)

Barua ya siri iliyokuja kiwekwa wazi hapo baadaye kutoka idara ya ujasusi ya Bulgaria kwenda kwa wababe wa Russia KGB alilalamikia ya kwamba matangazo ya radio ya Markov alilenga kukejeli serikali ya Bulgaria pamoja na kuchochea uasi ndani ya nchi.

Idara ya ujasusi ya Bulgaria ilianzisha jalada maalum la upelelezi dhidi ya Markov na hata baada ya kuhamia London bado alikuwa akipokea vitisho vya kumuua kupitia simu yake ya mezani.

Mwanvuli wa sumu
=========
Asubuhi ya tarehe 7 mwezi wa September mwaka 1978, bwana Georgi Markov alikuwa njiani akielekea kazini kwake mejengo ya ofisi za shirika la BBC. Wakati akiwa anasubiri kupanda bus akiwa pamoja na abiria wengine pale kituoni, ghafla akahisi maumivu ya ghafla na makali sana nyuma ya paja lake la kulia ambapo baadaye akaja kusema ni kama aling'atwa na mdudu tu.

Mtu aliyesimama karibu yake, ambaye alizungumza kiingereza kilichojawa na lafudhi ya kigeni, glafla akamsogelea na kuokota MWAMVULI uliokuwa umedondoka chini na kusha kusema kwa sauti ya chini sana "samahi sana mwamvuli wangu umekugonga kwa bahati mbaya". Kabla yule jamaa mwenye mwamvuli akapandacha taxi chaaaaap na gari kuwasha moto na kuondoka.

Baada ya kufika kazini na kujitazama kwa umakini zaidi, Markov akagundua kashimo kadogo, kekundu na kanakouma sana nyuma ya mguu wake ule. Kadri siku zilivyozidi kwenda alizidi kuumwa sana kisha kupelekwa hoapitalini akiugua homa kali sana. Bwana Georgi Markov akafariki mnamo tarehe 11 September.

Ripoti ya kitabibu ikaja kuonesha ya kwamba bwana Markov aliuwawa kwa punje ndogo iliyorushwa kama risasi katika mguu wake asubuhi ile ya majonzi. Baada ya uchunguzi wa maiti uliofuata, forensic pathologists wakaja kugundua punje ya chuma kidogo iliyokuwa na umbo na duara mbele ikiwa na ncha kama ya pini ikiwa imetumbukia ndani ya mguu wake.

Ile punje ya chuma ilirushwa kwa kutumia bunduki ya mwamvuli ikiwa imejazwa somo hatari sana aina ya Ricin yeye ujazo wa 0.2 milligrams kisha kufunikwa na nta ambayo alitengenezwa kuweza kuyeyuka katika joto la degree 37 Celsius (ambalo ndio joto la mwili wa mwanadamu) hivyo kufanya sumu ile kuanza kuchuruzika na kuingia ndani ya mtiririko wa damu.

Mashaka yakatanda ya kwamba kuna bunduki maalum yenye umbo kama la mwamvuli ilitumika kama silaha ya mauaji iliyopelekea kifo cha bwana Markov. Ingawa officer wa zamani wa KGB aliwahi kusema ya kwamba ni kweli KGB waliwahi kuwa na silaha na namna hiyo. Ingawa baadhi ya wachambuzi husema ya kwamba hiyo punje ya chuma ya sumu ya Ricin inaweza ikawa ilichomwa kwenye mguu wa Markov kwa peni maalum, kisha mwamvuli kuangushwa kwa makusudi kama zuga tu ili kupoteza ushahidi.

Ushahidi ukaja kuonesha ya kwamba mauaji ya bwana Markov yaliamriwa kutoka ngazi za juu kwa ushirikiano dhabiri wa idara za usalama za Bulgaria pamoja na Soviet KGB. Kabla ya mauaji haya ya mwaka 1978 idara ya usalama ya Bulgaria ilijaribu kuomba ushauri kutoka kwa mabigwa wazee wa kazi wa KGB juu ya njia gani nzuri ya kumzima (neutralize) Markov na KGB kuwapa mbinu mbili za hapo awali za kumaliza maisha yake.

Kwanza walitaka kunyunyuzia sumu ndani ya kinywaji chake katika sherehe ya chakula cha usiku pamoja na kutaka kupiga risasi alipoenda kimtembelea hawara yake ambapo majaribio yote mawili yalishindikana.

Ikaja kusadikika ya kwamba tarehe iliyochaguliwa ya kumuua kwa mara ya tatu, tarehe 7 September, ilikiwa ni tarehe ya kuzaliwa ya rais wa wakati huo wa Bulgaria na kifo cha Markov kuwa kama zawadi ya birthday kwa rais huyo.

Majalada yaliyokuja kuwekwa wazi hapo baadaye na idara ya usalama ya Bulgaria yalionesha ukaribu sana kati ya idara ya usalam ya nchi hiyo pamoja na mafundi wa KGB, ingawa wawakilishi wa KGB walikuwa makini sana kuhakikisha ya kuwa hawaacha alama yoyote wala kutambulika na wala wao kuhisishwa moja kwa moja na kifo cha bwana Markov.

Ingawaje files zinaonesha ya kuwa viongozi wa juu wa idara ya usalama wa taifa ya Bulgaria walienda Moscow miezi michache kabla ya mauaji ya bwana Markov ambapo mikakati ya kukuua Markov ilijadiliwa na wataamu wa kamati ya ufundi waliokuwa wakifanya kazi ndani ya maabara maalum za shirika la ujasusi la KGB.
=========
***MWISHO***

Post a Comment

0 Comments