Wasichana waliokamatwa Rehema Ndunguru (32) mkazi wa Sinza akiwa na mtuhumiwa mwenzake Moyo Ramadhani
Waziri Sitta, akiondoka Uwanja wa ndege wa Julius Nyerere.
Waziri Sitta, akisalimiana na baadhi ya viongozi wakati alipowasili Tazara.
--
Waziri
wa Uchukuzi, Mhe. Samuel Sitta jana alifanya ziara Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Shirika la Usafirishaji la Reli
(TAZARA) pamoja na Shirika la Usafirishaji la Reli (TRL) jijini Dar es
Salaam leo.
Katika ziara yake Waziri Sitta alikutana ana kwa ana na wadada wawili
wanaotuhumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya walioyokamatwa wakiwa
wameyameza aina ya heroini tayari kuyasafirisha kwenda mji wa hong Cong
Januari 25 kwa ndege ya Emirates kutokea uwanja huo.
Wadada hao wawili Rehema Ndunguru (32) mkazi wa Sinza mpaka jana alikwishatoa pipi 78
wakati mtuhumiwa mwenzake Moyo Ramadhani alikwishatoa pipi 86 ambapo
kazi ya kuwachunguza inaendelea.
Aidha
Waziri alikemea wanajishughulisha na biashara hiyo chafu huku akiwaonya
kamba mkono wake ni mrefu na atahakikisha anatimiza wajibu wake na
sheria kuchukua mkondo wake kwa wale wote wanaoojihusisha na biashara
hizo.
Waziri
Sitta alipoonana na wakina dada hao na kuwahoji hulipwa kiasi gani
walisema mpaka dola za kimarekani 6500 ambazo kwa fedha za Kitanzania ni
takribani shilingi 11,700,000.
0 Comments
Unapenda kuhabarika? Jiunge nasi Katika Twitter na Facebook ili tuhabarishane.
Kumbuka Kuacha maoni yako hapa pindi usomapo habari zetu. Karibu Tena