Header Ads Widget

Responsive Advertisement

VIJANA WATAKIWA KUSHIRIKI KOZI YA UDHIBITI WA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA JIJINI MWANZA.

 
Na George Binagi wa Mtanzania Media
Shirika la Rafiki Familiy Foundation la Mkoani Mwanza limetoa wito kwa watumiaji wote wa dawa za Kulevya Jijini Mwanza sanjari na wale walio katika Mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa, kujitoteza kwa wingi kwa ajili ya kushiriki kozi juu ya udhibiti wa dawa za kulevya.

Mbali na Kozi hiyopia Shirika hilo limeahidi kutoa matibabu kwa watu watakao bainika kuwa wameathirika zaidi na dawa hizo.

Hayo yalielezwa jana na
Dedory John Bugomola ambae ni Mratibu wa Shitika hilo wakati akizungumza na Radio Metro Fm na Mtanzaniamedia Blog kuhusiana na Semna hiyo ambayo inaanza rasmi leo baada ya zoezi la uandikishaji kufanyika jana.

Bugomola ametoa rai kwa Watu wote waliojiingiza katika utumiaji wa dawa za kulevya Jijini Mwanza sanjari na wale wanaotoka katika Mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa kujitokeza kwa wingi ili kushiriki kozi hiyo itakayodumu kwa muda wa majuma mawili kwa ajili ya kujinauru kutoka katika kifungo cha utumiaji wa dawa za kulevya.

Nae kijana Gabriel Kayegele ambae ni Mkazi wa Isamilo Jijini Mwanza ambae alikuwa mtumiaji wa dawa za kulevya kwa zaidi ya Miaka Sita iliyopita, amewasisitiza Vijana wenzake waliotumbukia katika utumiaji wa dawa za kulevya kujitokeza kwa wingi kushiriki katika kozi hiyo badala ya kuendelea kuteseka katika janga la utumiaji wa dawa hizo.

Deodory John Bugomola ambae ni Mratibu wa Shirika la Rafiki Family Foundation akitoa ufafanuzi katika picha mbele ya Kamera ya Mtanzaniamedia Blog juu ya aina mbalimbali za dawa za kulevya.
Gabriel Kayegele mkazi wa Isamilo Jijini Mwanza akiangalia aina mbalimbali za Dawa za Kulevya katika picha kama alivyokutwa na Kamera ya Mtanzaniamedia Blog akiwa katika Ofisi za Rafiki Family Foundation zilizopo Nyakato Jijini Mwanza.

Post a Comment

0 Comments