Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Video Review | #Kalima Br Kizo (Isaya)

Rorya Finest Blog Tunakuletea kipengele kipya kabisa ktika mtandao wetu kwa ajili ya kufanya Video Review kutoka sehemu mbalimbali Tanzania. Karibu ujiunge nasi. Mkoa wa Mara unazidi kukua kimuziki kadri siku zinavyozidi kwenda, Wasanii wanazidi kuongezeka na kuutangaza Mkoa wetu vizuri. Leo katika Video Review namleta kwenu Msanii Br Kizzo (Isaya wa Adorina) katika wimbo wake wa #Kalima, Video imetengenezwa na Saimako. Maudhui ya video ni mazuri na yanaendana na hali halisi katika maisha yetu ya kila siku. Isaya anamzungumzia mpenzi wake aitwae #Kalima, anamsihi asije akamuacha kwani maisha yanatafutwa na ipo siku watapata riziki yao. Isaya ni yatima na alilazimishwa kumuoa Kalima, hana uwezo hivyo amekwenda Mjini kutafuta maisha. Video hii haikupata Airtime ya kutosha katika Media za Tanzania na hilo ndo tatizo kubwa la Muziki wetu, wimbo ni mzuri lakini connection ya kufanya kazi nzuri kama hii ifike mbali inakua ndogo. Pata muda wa kuitazama hapa chini na unipe maoni yako.

Post a Comment

0 Comments