Header Ads Widget

Responsive Advertisement

SHILOLE x NUH MZIWANDA KWISHNEIII!!! | KILA MTU AMCHANA MWENZAKE

shilolee-3
Bongo Fleva na mwigizaji, Zuwena Mohammed a.k.a Shilole a.k.a Shishi Beiby na msanii mwenzake Nuh Mziwanda.



LILE penzi lililotikisa Bongo kati ya mwanadada mrembo ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na mwigizaji, Zuwena Mohammed a.k.a Shilole a.k.a Shishi Beiby na msanii mwenzake Nuh Mziwanda, limevunjika ghafla wikiendi iliyopita.
Awali, Shishi Beiby alikuwa amekolea kimahaba kwa ‘serengeti boy’ huyo na kulikuwa na kila dalili kwamba watafunga ndoa lakini mrembo huyo ndiye aliyekuwa kwa kwanza kutangaza juzi kwamba amempiga chini Nuh.
SHILOLE390
…Wakifanya yao.
Wikiendi iliyopita, wapenzi hao waliokuwa wameshibana na kugandana kama kupe, walionyesha kwamba wameachana vibaya, baada ya kutumia mitandao ya kijamii kutukanana, kitu ambacho wengi walikiponda na kudai wanatafuta kiki kwa lazima.
Championi lilipata taarifa hizo na kuamua kuwafungia kazi wote wawili na kuanza kumvutia waya Shishi Beiby ambaye alitoa ufafanuzi wa kile kinachoendelea kwenye uhusiano wao.
nuhu
Championi: Mambo vipi Shishi?
Shishi: Mambo poa tu mzima wewe?
Championi: Mi mzima aisee sijui kwa upande wako?
Shishi: Niko poa pia.
Championi: Vipi Ramadhani imeendaje?
Shishi: Kwanza kabisa ninamshukuru Mungu kwani tumemaliza salama funga yetu, lakini pia kupitia Mfungo wa Ramadhani kuna mambo mengi ambayo nimejifunza ikiwemo, kuswali, kupenda amani, kusamehe pamoja na kuwa na hofu ya Mungu. MZIWANDA2340 Championi: Vipi imekuwaje tena mbona nasikia umeachana na kaka yetu?
Shishi: Aisee ni kweli unajua Nuh ni mzinguaji, yaani licha ya kumsaidia lakini ananiletea ujinga daah! Acha afanye yake as longer as ni mwanaume na mimi ni mwanamke kila mtu atapata riziki yake mbele.
Championi: Kwani tatizo ni nini, maana mlikuwa kimya wenyewe imekuwaje?
Shilole: Kwa kweli mi siwezi kuzungumzia sana sababu ni mambo ya ndani kuachana naye ila we jua tu Nuh anazingua.
Championi : Ok! Basi poa, nikutakie siku njema.
Shilole: Asante na kwako pia.
UJUMBE ALIOUTUMA SHILOLE KWENYE INSTAGRAM
Shilolekiuno: Mwanaume hata umfanyie nini haridhiki lol! Pamoja na kukubali shida zake zote lakini mh! Nimejitahidi, nimehangaika ila sasa kama gari limewaka, akaaa babu weeh! Kanikuta na maisha yangu, wacha niendelee na maisha yangu, mimi na yeye baaaaaaasi #Gandalandizi. Alipotafutwa Nuhu alisema kwa kifupi: “Kuachana siyo jambo la kushangaza, kwa sababu wengi wanaachana na Mungu kapenda tuachane, kwa sasa nadili na kazi zangu tu.”
MUDA MFUPI BAADAYE NUHU NAYE AKATUPA JIWE M
ziwandanation: “Mwanaume wa kweli hukaa kimya, sibishani na upumbavu, mwanamke asiyeridhirika na kathaminiwa mpaka tatoo kachorwa na kuvumilia mambo yote aliyonifanyia ya kuniaibisha mbele ya mashabiki zangu, familia, wasanii wenzangu na wadau anaanza kunitukana mitandaoni for whaaat!!! mxeeeew mimi bado kijana na nina time ya kupata maisha yangu na mtu atakayethamini moyo wangu, nawaachia wanaume wenzangu na nyie mjaribu zari #Ashangedere.
ALICHOSEMA SHILOLE ALIPOZUNGUMZA NA CHAMPIONI WIKI MOJA ILIYOPITA KUHUSIANA NA PENZI LAKE KWA NUH
Jamani Nuh siyo mdogo ila ni mwili wake tu, lakini pia kama wanaona ni mdogo basi ni kwa upande wao na mtazamo wao, kama angekuwa mdogo mbona mimi ananiridhisha sana kwenye mambo yetu? Hakuna mfano, ndiyo maana tumetulizana.

Post a Comment

0 Comments