Header Ads Widget

Responsive Advertisement

Makala Maalum | BLACK WEDNESDAY: Nguvu ya Biashara ya Forex, Ujasusi na Yaliyo Nyuma ya Pazia - Episode II

Image result for forex
SEHEMU YA PILI


"…maisha hayajali kama uko sahihi au hauko sahihi. Bali maisha yanajengwa na kiasi gani cha faida unapata pale unapokuwa sahihi na kiasi gani cha hasara unapata pale unapokuwa hauko sahihi.."

- The Bold, 2017



GENESIS

Unapochunguza tukio lolote lile, usikimbilie kwenye hitimisho. Kwa sababu hata siku moja hakuna hitimisho linalotoa jawabu. Kila hitimisho ni muitikio akisi ya mjengeko wa chanzo au mizizi. Kwa hiyo ili kufahamu uhalisia wa suala lolote lile ni vyema kutazama matokeo yake lakini ni jambo la weledi zaidi kama ukizama na kufukua mzizi wake.

Kwa hiyo kabla sijaeleza namna ambavyo George Soros aliweza kuipigisha magoti nchi nzima ya Uingereza, kisa ambacho nitakitumia kujenga hoja zangu na maoni yangu juu ya biashara ya Forex ambayo imejizolea umaarufu hivi karibuni, kwanza kabisa nataka kutumia fursa hii kufukua mzizi wa tukio la Septemba 16, 1992 ambalo kwenye sehemu ya kwanza nilieleza kwamba Waziri Mkuu alikuwa ameitisha mkutano wa dharura nyumbani kwake Whitehall.

Ni kwamba,

Baada ya vita kuu ya pili ya Dunia, nchi za Ulaya ziliazimia kuunganisha uchumi wao kwa pamoja kwa mkazo zaidi.
Ikumbukwe kwamba ni miongo kama mitano tu nyuma kulikuwa kumemalizika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Vita hizi zote zilikuwa na hasara kubwa sana za kiuchumi. Kwa hiyo lengo kuu la kwanza la dhamira hii ya nchi za Ulaya kuunganisha chumi zao ilikuwa ni kujaribu kuzuia kutokea kwa vita kuu nyingine kwa maana ya kwamba, chumi hizi kama utatengenezwa mfumo wa kuziunganisha maana yake ni kwamba zitakuwa zinategemeana. Na kama zikitegemeana maana yake ni kwamba kila nchi itakuwa inawajibika zaidi kuepuka kutokea kwa vita nyingine ili kulinda uchumi wa nchi zao (yaani nchi yoyote katika jumuiya hiyo ikiingia vitani maana yake chumi za nchi nyingine zote ndani ya jumuiya nazo zitaathirika).
Kwa hiyo hill lilikuwa ni lengo kuu la kwanza kabisa.

Lengo la pili lilikuwa ni hatimaye kupatikane Umoja rasmi wa kisiasa na kidiplomasia ambao utachochea zaidi mshikamano wa nchi za Ulaya kiuchumi na hatimaye kuwa na uchumi ambao unaweza kushindana na nchi ya Marekani.

Wengi tunaifahamu EU (European Union) ya sasa ambayo ilianzishwa rasmi mwaka 1999. Lakini kwa kipindi hicho cha miaka baada ya Vita kuu ya pili ya Dunia, yaani mwaka 1957, nchi za Ulaya walianzisha chombo kinachoitwa European Economic Community (ECC). Kama ambavyo nilieleza awali, chombo hiki lengo lake kuu lilikuwa ni 'economic intergration.' Kujenga mafungamano ya kiuchumi baina ya nchi zote za Ulaya.

Sasa basi, mojawapo ya sera za kukumbukwa zaidi chini ya chombo hiki ilikuwa ni uanzishwaji wa mfumo wa ERM (European Exchange Rate Mechanism). Sera hii ilianza kutekelezwa rasmi mwaka 1979.

Kipindi ambacho nchi hizi ziliungana kuanzisha chomo hiki cha uchumi kulikuwa na pendekezo la kuwa na sarafu moja. Lakini nchi nyingi hazikuwa tayari kuachilia sarafu zao na kuanza kutumia sarafu mpya.
Kwa hiyo mwaka huu 1979 walipoanzisha sera ya ERM walikubaliana kwamba kila nchi itaweka thamani ya sarafu yake kulingana na thamani za sarafu za nchi nyingine ndani ya Ulaya.

Kwa kawaida, thamani ya sarafu ya nchi inatokana na namna 'inavyoperform' kwenye soko kwa kuzingatia kanuni za 'demand and supply'. Thamani yake itapanda au kushuka kutokana na namna inavyohitajika na upatikanaji wake.


Lakini nchi za Ulaya zenyewe kipindi hicho kwa kuona wingi wao wa nchi wanachama, walidhamiria kulinda thamani za sarafu zao.

Sasa basi, kwa kuwa Ujerumani ndio ambayo ilikiwa na uchumi mkubwa zaidi na imara, kwa hiyo sarafu za nchi zote kwenye jumuiya zilitakiwa kuweka thamani yake kulingana na thamani ya fedha ya Ujerumani ambayo kipindi hicho walikuwa bado wanatumia Deutschmark (DM).

Kuna jambo moja la muhimu ambalo tunapaswa kuliweka akilini. Pale ambapo serikali inakuwa inaamua kufuata mfumo huu wa kuweka 'fixed exchange rates' inapaswa pia kushiriki moja kwa moja kwenye soka la biashara ya fedha. Kivipi?
Unapoacha sarafu yako 'ifloat' kwenye soko, maana yake ni kwamba soko ndilo litaamua kiwango cha 'exchange rate' ya sarafu yako dhidi ya sarafu za nchi nyingine. Hii ni tofauti kabisa na kama ukiamua kuwa na 'fixed exchange rate'. Unapswa kujihusisha muda wote kwenye soko ili kuhakikisha 'exchange rate' inabaki pale ambako unataka.

Hii ikoje?

Tuseme kwa mfano nchi imeweka 'exchange rate' yake katika kiwango fulani. Sasa kuna namna mbili ambazo serikali (benki kuu) ambayo imeamua kuwa na fixed exchange rate wanakuwa wanafanya ili kiwango hicho kibakie pale.

Moja ni kushiriki na kwa kuuza na kununua sarafu yao kwenye soko. Serikali inaweza kuamua kuweka fixed exchange rate lakini soko nalo linatoa presha kwa kiwango hicho kilichowekwa eidha kama ni kikubwa sana au kidogo sana kwa kuzingatia kanuni ya 'demand and supply' ya sarafu husika. Kwa hiyo mara kadhaa soko la fedha la dunia litatoa presha kwa kiwango hiki fixed kiweze kubadilika. Sasa serikali wanachofanya ni kuuza au kuinunua sarafu yao. Kwa mfano kama kukiwa na presha ya sarafu kushuka chini ya kiwango kile cha exchange rate ambacho wamekiweka, serikali itatumia hazina yake ya fedha ya kigeni kuinunua sarafu yake. Hii itasababisha thamani ya sarafu husika kupanda kutokana na 'supply' kuwa ndogo na hatimaye kiwango cha exchange rate kubaki pale ambako serikali imeweka.

Pia ikitokea kwamba kuna presha ya exchange rate kupanda kuzidi pale ambapo serikali wameweka, kinachofanyika serikali yenyewe inaanza kuiuza sarafu yake. Hii itafanya thamani ya sarafu husika kushuka kutokana na 'supply' kuwa kubwa na hivyo exchange rate inarudi pale ambako serikali inataka.

Njia ya pili ambayo serikali ambayo inayoweka fixed exchange rate wanashiriki kwenye soko ili exchange rate ibaki pale pale ni kwa kucheza na Interest Rates. 
Kwa mfano serikali ikitaka sarafu yake ipande thamani wanachoweza kufanya ni kuongeza Interest Rates. Unapoongeza Interest Rates maana yake ni kwamba mabenki, mashirika makubwa ya fedha na wenye mitaji mikubwa watanunua zaidi sarafu yako ili waweze kuikopesha kwa faida kubwa (umeongeza interest rates). Lakini pia kama ukitaka thamani ya sarafu yako ishuke, unachofanya unaweza kushusha interest rates. Maana yake ni kwamba mabenki na wenye mitaji mikubwa ya fedha watapunguza kununua sarafu yako na kwenda kununua sarafu nyingine zenye rates za juu. Hii itafanya sarafu yako kushuka thamani.

Huu mchezo wa kucheza na interest rates ni adhimu sana kwa serikali zote duniani. Ni moja ya turufu adhimu zaidi ambayo serikali wanayo ili kurekebisha uelekeo wa kiuchumi. Kwa mfano kama nchi ikiwa kwenye mdororo wa kiuchumi, serikali inaweza kushusha interest rates ili kuchochea uwekezaji na matumizi (spending). Au kwa mfano kukitokea mfumuko mkubwa wa bei (inflation), serikali inaweza kuongeza interest rates ili kupunguza mzunguko wa fedha na hivyo kuongeza demand ya sarafu yao na kufanya inflation kwenda chini.


Nadhani unapata picha walau kidogo ni namna gani pale serikali ikiamua kuwa na 'fixed exchange rates' inapaswa kuhusika kwa kiwango kikubwa mno katika soko la dunia la fedha. Ni suala ambalo kama serikali halitalifanya kwa makini, kosa dogo tu linaweza kuzamisha uchumi wa nchi.

[​IMG]
Waziri Mkuu Margaret Thatcher na Rais Regan wa Marekani


Hii inatupeleka mpaka mwaka 1990. Katika kipindi hiki nchi ya Uingereza ilikuwa inapitia kwenye moja ya vipindi vigumu zaidi vya kiuchumi. Mfumuko wa bei ulikuwa mkubwa, uzalishaji umeshuka kwa kiwango kikubwa na uuzaji wa bidhaa nje umeporomoka. Mbaya zaidi serikali ilikuwa inaonekana kwamba hawakuwa na uwezo wa kutatua mdororo huu wa kiuchumi.

Ikumbukwe kwamba mpaka kipindi hiki, nchi ya Uingereza bado ilikuwa haijajiunga na mpango wa ERM. Kwa hiyo zilianza kelele nyingi za wanasiasa kushinikiza serikali waingie kwenye mpango wa ERM kama ilivyo kwa nchi nyingine za Ulaya na labda inaweza kusaidia kufufua kwa kasi tena uchumi wa nchi yao.

Waziri Mkuu wa Uingereza wa kipindi hicho Bi. Margaret Thatcher alikuwa anapinga vikali mpango huu wa ERM. Alikuwa anaamini kwamba viwango vya exchange rate vinapaswa kujiweka vyenyewe kutokana muelekeo wa soko badala ya serikali kuingilia na kuweka viwango 'fixed.'
Ubaya ni kwamba hali ya kiuchumi haikuwa nzuri na wananchi wa Uingereza hawakuwa na imani na serikali kama walikuwa na uwezo wa kuwaondoa kwenye mdororo huo.

Kwa kifupi Bi. Margaret Thatcher hakuwa na 'mtaji' wa kisiasa kushawishi wananchi na hata mawaziri wake kwamba Uingereza isiingie kwenye mpango wa ERM. Kulikuwa na sauti nyingi sana za watu wazito lakini sauti ambayo ilikuwa kinara zaidi katika kushinikiza Uingereza kuingia kwenye mpangobwa ERam alikuea ni Waziri wa Fedha wa kipindi hicho Bw. John Major (huyu ndiye alikuja kuwa Waziri Mkuu baadae) yeye na wenzake wote walitaka Uingereza kuingia kwenye mpango wa ERM.
Kutokana ma msukumonwa kisiasa na uchumi kuendelea kudorora hatimaye mwezi Octoba, 1990 nchi ya Uingereza ikaingia kwenye mpango wa ERM.

Kama ambavyo nilieleza pale awali kwambwa kwa kuwa uchumi wa Ujerumani ulikuwa ndio mkubwa na imara kuliko chumi nyingine zote kwa hiyo thamani za sarafu zote za nchi zote wanachama vilipewa thamani kutokana na Deutsh Mark (DM) ya Ujerumani.
Uingereza yenyewe ilipojiunga Paundi yake ilipewa thamani ya 2.95 DM. Yaani Paundi moja ya Uingereza ni sawa na 2.95 DM za Ujerumani. Pamoja na hilo serikali ya Uingereza walitakiwa wahakikishe kuwa kwa kipindi chote thamani ya Paundi haitoki kati ya 2.78 DM mpaka 3.13 DM.

Haukupita muda mrefu, John Mayor ambaye ndiye alikuwa mstari wa mbele kushawishi Uingereza kuingia kwenye mpango wa ERM alishika madaraka ya Uwaziri Mkuu kuchukua nafazi ya Bi. Margaeret Thatcher.

Muda si muda mambo yaakanza kwenda sawia. Hiyo ilikuwa ni mwaka mwishoni mwa 1990 na mwaka 1991 na mwanzoni mwa mwaka 1992.
Mfumuko wa bei ulishuka, interest rest zikaaa kwenye mstari na kiwango cha wasio na ajira kilikuwa chini kabisa kwenye kiwango cha kihistoria. Kwa kifupi mambo yalikuwa swadakta kabisa. Waziri Mkuu mpya Mhe. John Mayor akaonekana shujaa machoni kwa Waingereza na kiongozi wa kupigiwa mfano duniani.

[​IMG]
Waziri Mkuu John Major


Wakati huo huo, Jijini New York

Kuna msemo wa waswahili wanasema kwamba, wewe ukijua ya mbele, wenzako wanajua ya pembeni… na wewe ukijua ya pembeni basi wenzako wanajua ya nyuma.

Hiki ndicho ambacho kilikuwa kinatokea 

Jijini New York nchini Marekani katika ofisi maridadi za Kampuni ya Quatumn Fund alikuwa ameketi mtu ambaye kwa sasa hakuna ambaye alikuwa qnamjua au anamfuatilia kwa sasa. George Soros alikuwa anafuatilia hatua kwa hatua kile ambacho kilikuwa kinaendelea nchini Uingereza.

Wakati Waingereza wakiwa wanafurahi na kushangilia uchumi wao kutengamaa… huko jijini New York, kulikuwa na sisila, George Soros ambaye mpaka muda huu pengine ndiye alikuwa mtu pekee duniani aliyeona 'loop hole' katika hali hii ya "kutengemaa kwa uchumi" kwa Uingereza. Alikuwa ameusoma mchezo wote hatua kwa hatua… kwa hiyo ndio maana wakati Waingereza wakishangilia na Dunia ikimpongeza Waziri Mkuu John Mayor, wakati ambao hata watu wa serikali wenyewe, baraza la mawaziri na wataalamu wao wakiona neema na kuwafamya wapongezane kwa kugongesha glass… yeye George Soros hakuona 'kushamiri kwa uchumi' bali aliona 'limbo', shimo refu la giza… na alidhamiria kutengeneza mpango maridhawa kabisa na kuitumbukiza nchi ya Uingereza kwenye shimo hilo. Pia alitaka kutumia fursa hii kuandika jina lake kwenye vitabu vya historia kwa vizazi na vizazi kwa karne kadhaa zijazo.



Chiefs, tupate kifungua kinywa kwanza… tutaendelea.

Inaendelea....

Imeandaliwa na The Bold | Jamii Forums

Post a Comment

0 Comments